• HABARI MPYA

    Wednesday, October 15, 2014

    MICHO: TATIZO AFRIKA MASHARIKI HATUNA UMOJA, TUNAANGUSHANA WENYEWE KWA WENYEWE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa Uganda, Milutin Sredojevich ‘Micho’ amesema Afrika Mashariki hakuna umoja, jambo ambalo linachangia kuzorota kwa maendeleo ya soka katika ukanda huu.
    Uganda ilifungwa 1-0 na Togo katika mchezo wa Kundi E kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco na Micho akamlaumu refa wa Kenya, Davies Omweno kutoitendea haki The Cranes.
    “Kama angekuwa muungwana, (Jumamosi) angetupa hata penalti moja kama si zaidi, ilitokea kabisa tulistahili kupewa (penalti), lakini hakufanya hivyo,”amesema Micho mwishoni mwa wiki kutoka Kampala.
    Micho amelalamikia Afrika Mashariki kutokuwa na umoja kiasi cha kumalizana wenyewe kwa wenyewe jambo ambalo linachangia ukanda huu kutokuwa na mafanikio katika soka

    Mserbia huyo amesema kwamba Afrika Magharibi wanapiga hatua kubwa kimaendeleo katika soka kwa sababu pia pamoja na umoja wao walionao. “Kwangu hii si mara ya kwanza nikiwa na Uganda marefa wa Afrika Mashariki wananiangusha, lazima tubadilike,”amesema.
    Micho anaiongoza Uganda leo katika mchezo wa ugenini na Togo mjini Lome, ikihitaji ushindi ili kujiweka sawa kwenye mbio za Morocco mwakani.
    Kwa sasa, Cranes yenye pointi nne inashika nafasi ya pili nyuma ya Ghana yenye pointi tano kwenye kundi hilo, wakati Togo ina pointi tatu tu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MICHO: TATIZO AFRIKA MASHARIKI HATUNA UMOJA, TUNAANGUSHANA WENYEWE KWA WENYEWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top