• HABARI MPYA

    Sunday, June 15, 2014

    MSHAMBULIAJI TEGEMEO BRAZIL, HULK AUMIA MISULI MAZOEZINI LEO

    MSHAMBULIAJI wa kwanza wa Brazil, Hulk aliondoka kwenye mazoezi ya timu yake akiwa anasumbuliwa na maumivu ya misuli ya mguu wake wa kushoto.
    Hulk, ambaye alianza pamoja na Neymar na Fred katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia dhidi ya Croatia, alifanya mazoezi kwa dakika zisizozidi 15 leo kabla ya kuumia na kutoka. 
    Alikwenda kuketi benchi na baada ya muda kidogo akachukuliwa na mmoja wa madaktari wa timu hiyo kwenda kwenye chumba maalum kwa uchunguzi. Baada ya kuifunga Croatia 3-1 Alhamisi, Brazil itarudi uwanjani Jumanne kumenyana na Mexico.  

    Shakani: Hulk (kulia) alifanya mazoezi kwa dakika zisizozidi 15 na kikosi cha Brazil kabla ya kuumia
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSHAMBULIAJI TEGEMEO BRAZIL, HULK AUMIA MISULI MAZOEZINI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top