• HABARI MPYA

    Tuesday, June 17, 2014

    MAREKANI YAICHAPA GHANA 2-1, AFRIKA MWAKA HUU UROJO KOMBE LA DUNIA

    MAREKANI imeendeleza kilo kwa timu za Afrika, baada ya usiku wa kuamkia leo kuifunga Ghana mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi G Kombe la Dunia nchini Brazil.
    Shukrani kwao, Clint Dempsey aliyefunga bao la kwanza sekunde ya 31 baada ya kuwachambua mabeki wa Ghana na John Brooks aliyefunga la pili kwa kichwa dakika ya 86.
    Mshambuliaji huyo wa zamani wa Fulham, aliifungia timu ya Jurgen Klinsmann bao kla ushindi dkika nne tu tangu Andre Ayew aisawazishie Ghana.
    Kikosi cha Ghana kilikuwa; Kwarasey, Opare, Mensah, Boye, Asamoah, Atsu/Adomah dk78, Rabiu/Essien dk71, Muntari, Andre Ayew, Jordan Ayew/Boateng dk59 na Gyan.
    Marekani: Howard, Johnson, Cameron, Besler/Brooks dk46, Beasley, Bedoya/Zusi dk77, Jones, Bradley, Beckerman, Dempsey, Altidore/Johannsson dk23.
    Mwanzo mzuri Marekani: Clint Dempsey akishangilia baada ya kuifungia Marekani dhidi ya Ghana
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAREKANI YAICHAPA GHANA 2-1, AFRIKA MWAKA HUU UROJO KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top