JAMAL Emil Malinzi aligombea Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mara mbili, mara ya kwanza alishindwa na Leodegar Chillah Tenga.
Alipojaribu kurejea kugombea tena, akawekewa vikwazo kibao hadi akalazimika kufuata taratibu za kuondoa vikwazo hivyo.
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) linakataza masuala ya mchezo huo kupelekwa kwenye mahakama za dola na limejiwekea utaratibu wake mzuri kuhakikisha matatizo yote yanapatiwa suluhu ndani ya mfumo wake.
Malinzi alilitambua hilo na akaliheshimu, akaanza kufuata taratibu zile zile ambazo FIFA wameziweka hadi akafanikiwa kuondolewa vipingamizi na akagombea tena mwaka jana.
Alimshinda Athumani Jumanne Nyamlani na kufanikiwa kuwa rais mpya wa TFF.
Iko wazi, kupeleka masuala ya soka mahakamani ni kosa na adhabu yake kubwa unapofanya hivyo unaondolewa kwenye familia ya soka- unatengwa kabisa.
Mjadala mkubwa katika soka ya Tanzania kwa sasa ni sakata la mgombea Urais wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Michael Richard Wambura ambaye Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo ilimzuia kugombea kwa sababu aliwahi kuipeleka klabu hiyo mahakamani.
Hata hivyo, Kamati ya Rufani ya TFF chini ya Rais Malinzi imetengua maamuzi hayo na kumrudisha kwenye mbio za kuwania uongozi wa Wekundu wa Msimbazi.
Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti, Wakili Julius Lugaziya mwana Yanga mzuri, imesema imemrejesha Wambura kwa sababu baada ya kosa alilofanya aliendelea kulipia kadi yake na kushiriki mikutano hata kuteuliwa kwenye Kamati ya Utendaji ya klabu.
Ni kweli, Wambura aliendelea kulipia ada za uanachama na kushiriki mikutano ya klabu, pia akateuliwa na Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Simba SC Alhaj Ismail Aden Rage kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji.
Rage alimteua Wambura wakati ambao klabu hiyo ipo katika mgogoro, huku sababu akiwa ni yeye mwenyewe kupingwa na wanachama, kiasi cha kufikia Wajumbe wa Kamati yake ya Utendaji kufanya mkutano na kutangaza kumsimamisha.
Wakati uamuzi huo unafikiwa na kumteua mzee Joseph Itang’are ‘Kinesi’ kuwa kaimu Mwenyekiti, Rage alikuwa nje ya nchi kwa shughuli za kisiasa. Rage pia ni Mbunge wa Tabora mjini CCM.
Wazi kikao cha kumsimamisha Rage kilikuwa batili na aliporejea nchini, kiungo huyo wa zamani wa Simba SC akaamua kufanya kile kitu watu wa mjini wanasema; “kumwaga ugali, baada ya wenzake kumwaga mboga”.
Rage akatangaza kuwasimamisha wote walioshiriki kikao kile na kumteua Wambura kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji.
Rage alifanya hivyo akijua fika Wambura ni mwanachama batili, lakini kwa kuwa alikuwa anatafuta watu wa kumuunga mkono nje ya upande unaompinga, akaona Katibu mwenzake huyo wa zamani wa FAT ni mtu sahihi.
Huwezi kupata lugha nyingine ya kuyaita haya mambo zaidi ya ‘uhuni’- katiba zinakiukwa na mambo yanaamuliwa kienyeji, matokeo yake soka yetu inaendelea kuwa vurugu tupu.
Inafahamika wazi, katika harakati za Malinzi kugombea Urais wa TFF, alikuwa bega kwa bega na Wambura na baada ya kushinda, wengi walitabiri atampa Ukatibu wa kuajiriwa.
Lakini kinachojitokeza sasa ni tofauti na dhana ya wengi, ni kama Malinzi ameamua kumsaidia Wambura kuhakikisha kwanza anagombea Urais wa Simba SC.
Sasa, Malinzi naye anaingia katika mtego wa kuvunja Katiba, jambo ambalo mbele ya safari ni hatari kwake.
Kwa sasa, Malinzi anaamini idadi kubwa ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF ni wake kwa kuwa ni ‘juzi tu’ walimuwezesha kumshinda Nyamlani katika uchaguzi.
Ila akae akijua kwamba, kitendo cha kumbeba Wambura ni ukiukwaji wa Katiba na dhambi hiyo itakuja kumhukumu siku moja.
Tunahitaji kuwa waadilifu, kwa kuongoza soka kwa misingi ya Katiba ili kujenga nidhamu katika mchezo huo nchini. Kujaribu kutaka kuhalalisha mambo ambayo si halali ni kufungua milango ya vurugu zaidi- kwani wengine siku nyingine watakwenda mahakamani, na katika utetezi wao, watasema; “Mbona Wambura”.
Haimuathiri Malinzi kwa sasa, lakini ikitokea mtu akaenda mahakamani katika mapambano na yeye, ndipo atauona umuhimu wa kufuata Katiba.
Hakuna asiyejua masuala ya soka hayapelekwi mahakamani kwa kuwa FIFA haitaki na Wambura anajua alifanya kosa kubwa.
Malinzi hadi kusafiri kwenda Zurich, Uswisi yalipo makao makuu ya FIFA hakuzuiona mahakama hapa Tanzania ambazo Wambura alikwenda?
Malinzi arudi nyuma na aone umuhimu wa kuheshimu miiko iliyowekwa na FIFA na kumtendea haki tu swahiba wake Wambura, ili kutoa fundisho kwa watu wengine pia siku nyingine, wasithubutu hata kufikiria kufanya kitu kama hicho. Wasalam. Naitwa Mahmoud Ramadhani Zubeiry, au unawza kuniita BIN ZUBEIRY.

.png)
0 comments:
Post a Comment