Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesimamisha mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Simba SC hadi hapo klabu hiyo itakapounda Kamati ya Maadili ambayo itasikiliza masuala ya kimaadili kuelekea uchaguzi huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya TFF, katikati ya Jiji la Dar es Salaam mchana wa leo, rais wa TFF, Jamal Emil Malinzi amesema kwamba Simba SC inatakiwa kuwa imekwishaunda Kamati ya Maadili hadi kufika Juni 30, mwaka huu.
![]() |
| Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesimamisha uchaguzi wa Simba SC |
Malinzi amesema kwamba hatua hiyo imefuatia TFF kupokea malalamiko mengi juu ya ukiukwaji wa maadili kwa baadhi ya wagombea na wanachama wa klabu hiyo.
Malinzi amesema kwamba baada ya kuundwa kwa Kamati hiyo Maadili itasikiliza malalamiko yote ya kimaadili yanayougubika mchakato wa udhaguzi huo, ambao awali ulipangwa kufanyika Juni 29, mwaka huu.
Malinzi amesema kwamba kwa sasa Kamati ya Utendaji ya Simba SC iliyopo madarakani chini ya Mwenyeiiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage itaendelea kuiongoza klabu hiyo hadi hapo mchakato wa uchaguzi utakapokamilika.



.png)
0 comments:
Post a Comment