• HABARI MPYA

    Sunday, June 15, 2014

    STARS KWENDA BOTSWANA JUNI 24 KUWEKA KAMBI YA KUKUSANYA NGUVU ZA KUUA MAMBA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini wiki ijayo kwenda Botswana kuweka kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na mchezo dhidi ya Msumbiji kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Morocco.
    Wachezaji wote wa Taifa Stars waliruhusiwa kurejea makwao jana kwa ajili ya kujiandaa na safari hiyo na watakutana tena kesho.
    Kikosi cha Stars kilichoitoa Msumbiji

    Stars inayofundishwa na Mholanzi, Mart Nooij itaondoka nchini Juni 27 kwenda Gaborone, ambako itaweka kambi ya mazoezi hadi Julai 7 itakaporejea nchini.  
    Taifa Stars itamenyana na Msumbiji ‘Mambas’ katika hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco baada ya kuitoa Zimbabwe juzi kwa jumla ya mabao 3-2, ikianza kwa ushindi wa 1-0  nyumbani na kumaliza kwa sare ya 2-2 juzi mjini hapa.
    Mechi yake kwanza itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Julai 19 na 20 mwaka huu, wakati mechi ya marudiano itafanyika Msumbiji kati ya Agosti 2 na 3 mwaka huu. 
    Stars pia inatarajiwa kuwa na mchezo wa kujipima nguvu na Uganda kabla ya kumenyana na Msumbiji.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS KWENDA BOTSWANA JUNI 24 KUWEKA KAMBI YA KUKUSANYA NGUVU ZA KUUA MAMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top