• HABARI MPYA

    Friday, June 13, 2014

    DAVID LUIZ ASAINI MIAKA MITANO PSG

    BEKI David Luiz amekamilisha uhamisho wake kutoka Chelsea kutua Paris St Germain kwa kusaini Mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ufaransa.
    Luiz - ambaye aliichezea Selecao jana katika mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia ikishinda 3-1 dhidi ya Croatia anaondoka Stamford Bridge kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 50, hivyo anakuwa beki ghali zaidi duniani.
    Klabu hiyo ya Ufaransa imetangaza katika tovuti yake kwamba; "Paris Saint-Germain inayo furaha kutangaza kukamilisha usajii wa mwanasoka wa kimataifa wa Brazil, David Luiz kutoka Chelsea FC, atakayekuwa wetu kwa miaka mitano ijayo,".
    Shangwe za ushindi wa jana: David Luiz akishangilia ushindi wa jana wa Brazil. Beki huyo amesaini mkataba wa miaka mitano PSG
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DAVID LUIZ ASAINI MIAKA MITANO PSG Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top