MECHI ya kwanza ya Kundi B Kombe la Dunia inaanza muda mfupi toka sasa na vikosi vya timu zote mbili mabingwa watetezi Hispania na Uholanzi vimetajwa.
Hii inachukuliwa kama mechi ya kisasi baada ya timu hizo zilizokutana katika fainali ya michuano hiyo miaka minne iliyopita Afrika Kusini na bao pekee la Andres Iniesta likaipa ubingwa Hispania.
Kisasi leo? Nigel de Jong wa Uholanzi akimpiga teke la kung'fu Xabi Alonso wa Hispania. Wawili hao wote wanaanza leo, je wataendeleza uadui wao? |
Lakini pia tukio la mchezaji wa Uholanzi, Nigel de Jong kumpiga teke la kung'fu mchezaji wa Hispania, Xabi Alonso linatarajiwa kukumbushia uhasama wa wachezaji hao ambao wote wamepangwa kuanza.
Kikosi cha Uholanzi ni; Cillessen, Vlaar, De Vrij, Martins Indi, Blind, De Jong, Janmaat, De Guzman, Van Persie, Sneijder na Robben.
Hispania; Casillas, Pique, Iniesta, Xavi, Alonso, Sergio Ramos, Busquets, Alba, Costa, Silva na Azpilicueta.
0 comments:
Post a Comment