SHERIA ya teknolojia langoni hatimaye leo imetumika kikamilifu kumaliza utata wa bao Ufaransa ikiitandika mabao 3-0 Honduras katika mchezo wa Kundi E Kombe la Dunia. Karim Benzema amefunga mabao mawili mjini Porto Alegre dakika za 45 kwa penalti na 72, wakati bao lingine Noel Valladares alijifunga dakika ya 48 na kulazimika sheria ya teknolojia kwenye mstari wa goli kutumika ili kuhakikisha kama lilikuwa bao halali.
Wilson Palacios wa Honduras alionyeshwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu baada ya kumsukuma Paul Pogba kwenye boksi na Benzema akafungwa kwa penalti.
Kikosi cha Ufaransa kilikuwa; Lloris, Debuchy, Varane, Sakho, Evra, Pogba/Sissoko dk57, Cabaye/Mavuba dk65, Matuidi, Valbuena/Giroud dk78, Benzema na Griezmann.
Honduras: Valladares, Beckeles, Bernardez/Osman Chavez dk46, Figueroa, Izaguirre, Najar/Claros dk58, Wilson Palacios, Garrido, Espinoza, Bengtson/Boniek Garcia dk46 na Costly.



.png)
0 comments:
Post a Comment