Na Prince Akbar, Dar es Salaam
KATIBU wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Hicham El Amrani ameitaka Rwanda kuendelea na kazi nzuri ya maandalizi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwaka 2016, michuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
El Amrani alitoa maneno hayo baada ya kutembelea viwanja ambayo vitatumika kwa ajili ya michuano hiyo Jumanne ya Aprili 8, mwaka 2014.
Msafara huo uliongozwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou aliyeambatana na Makamu wake wa Pili, Almamy Kabele Camara, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya CHAN.
Waziri wa Michezo na Utamaduni wa Rwanda, Protais Mitali na Waziri wa Miundombinu, Silas Lwakabamba na Degaule Vincent Nzamwita, Rais wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) pia walikuwepo.
Viwanja vilivyotembelewa na kuidhinishwa ni pamoja na Huye, Rubavu na Kigali ambako kuna viwanja viwili, Amahoro na Kigali.
Msafara wa CAF baadaye ulikutana na Kamati ya ndani ya Maandalizi kujadili masuala mbalimbali kuhusu michuano hiyo.
El Amrani alisema: “Rwanda ipo katika njia sahihi kuandaa michuano hii mwaka 2016 na tunajivunia kwa sababu tulikuwa na Waziri wa Michezo na Utamaduni pamoja wa Miundombinu pamoja nasi wakati tunatembelea viwanja mbalimbali vitakavyotumika kwa mashindano hayo na hii inaonyesha ushirikiano wa hali ya juu,”.
“Tunafahamu kwamba wakati Rais Paul Kagame anapoahidi kitu, anatimiza na Rwanda wakati wote imekuwa ikifanikiwa na hii ilithibitishwa na mlipoandaa Fainali za vijana chini ya miaka 20 mwaka 2009 na U17 mwaka 2011 na hakuna sababu kwa nini msiwe tayari kwa ajili ya CHAN,”alisema.
Michuano ya CHAN iliyoanzishwa maalum kuwakutanisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee ilifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2009 nchini Ivory Coast, Sudan mwaka 2011 wakati mwaka huu imefanyika Afrika Kusini.

![]() |
Viongozi wa CAF wakiwa na viongozi wa Rwanda mjini Kigali |

0 comments:
Post a Comment