IMEWEKWA SEPTEMBA 2, 2013 SAA 2:48 ASUBUHI
KLABU ya Arsenal imetoa ofa ya Pauni Milioni 40 kwa ajili ya kiungo wa Real Madrid, Mesut Ozil lakini inaweza kukabiliana na ushindani kutoka Paris Saint-Germain na Manchester United katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho.
Nyota huyo wa Ujerumani, alibaki kwenye benchi wakati Real inashinda 3-1 dhidi ya Athletic Bilbao Jumapili, kama ilivyokuwa kwa mchezaji mwingine anayetakiwa na Manchester United, kiungo wa Athletic, Ander Herrera.
Ozil alionekana aliyechanganyikiwa akiwa ameketi karibu na Iker Casillas kwenye benchi na binafsi ameweka wazi anataka kuondoka Bernabeu, kutokana na kuhofia kupoteza namba kwa ujio wa Gareth Bale.
Anakwenda England? Mesut Ozil aliachwa benchi Real Madrid huku Arsenal ikiwa inamtaka
Arsenal ilianzisha mazungumzo Ijumaa na wanatumai kufika mshahara wa Ozil, Pauni 180,000 kwa wiki ili kukidhi kiu ya mashabiki wake kusajili mchezaji wa kiwango cha dunia.
Pamoja na hayo wanakabiliwa na ushindani kutoka Paris Saint-Germain, ambao walituma maombi yao Jumapili, na United, ambako wanataka kupeleka ofa ya pili baada ya awali kusema Ozil si aina ya mchezaji wanayemtaka.
Ozil yuko tayari kutua England na Arsenal au United mojawapo inaweza kumfaa.
Mchezeshaji: Ozil anaweza kuchagua kusaini PSG au Manchester United
Arsenal pia imeonyesha nia ya kumsajili winga wa Real, Angel Di Maria wakati kiungo wa vigogo hao wa Hispania, Kaka ametolewa ofa kwao, lakini wanaendelea kuzungumza na AC Milan.
Arsenal imekubali kumsajili kwa mkopo wa muda mrefu, kipa wa Palermo, Emiliano Viviano. Kipa huyo wa kimataifa wa Italia alikuwa kwa mkopo Fiorentina msimu uliopita na alikwenda London Jumapili tayari kwa vipimo vya afya asubuhi ya leo.
Mshambuliaji wa Palermo na Uruguay, Abel Hernandez naye anatakiwa na Arsenal, inayomtaka pia 'mwananchi mwenzake', Luis Suarez, wakati usajili wa mkopo wa mshambuliaji wa Chelsea, Demba Ba pia unawezekana.
Anaondoka: Angel Di Maria pia anaweza kuondoka Real Madrid


.png)