• HABARI MPYA

    Thursday, April 11, 2013

    SIR ALEX FERGUSON APIGA HATUA KUBWA KATIKA KUWANIA SAINI YA MKALI WA MABAO RADAMEL FALCAO ANAYEZITOA UDENDA MAN CITY NA CHELSEA PIA


    KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amejiunga kwenye mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Atletico Madrid mwenye thamani ya Pauni Milioni 47, Radamel Falcao. 
    Manchester City na Chelsea wote wamehusishwa kwa kiasi kikubwa kumuwania Falcao, ambaye amejijengea umaarufu kama wa washambuliaji wakubwa duniani kwa kuifungia mabao 54 Atletico tangu ajiunge nayo akitokea  Porto mwaka 2011. 
    Plot: Manchester United will enter the race to sign Atletico Madrid star Radamel Falcao
    Kifaa: Manchester United itaingia kwenye mbio za kuwania saini ya nyota wa Atletico Madrid, Radamel Falcao
    Radamel Falcao
    Radamel Falcao
    Lakini inafahamika kwamba United imejitosa kwenye mbio za kumuwania mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia mwenye umri wa miaka 27 na inajiandaa kumruhusu Javier Hernandez ahamie Madrid kama sehemu ya dili hilo. 
    Vinara hao wa Ligi Kuu England wako tayari kutoa Pauni Milioni 47 kwa ajili ya Falcao, wakiipa ofa ya Pauni Milioni 27 taslimu klabu hiyo ya Hispania pamoja na Hernandez ambaye thamani yake ni Pauni Milioni 20. 
    Pamoja na hayo, taarifa nchini Hispania zinasema kwamba tayari malipo taslimu yamekwishafanyika, na inaaminika kwamba United ipo katika hatua za awali za kutimiza ndoto zake za kumnasa mkali huyo wa mabao.
    Swap deal: Javier Hernandez could make way for Falcao as Manchester United prepare a bid for Falcao
    Dili la kubadilishana wachezaji: Javier Hernandez anaweza kwenda kuchukua nafasi ya Falcao huku Manchester United ikijiandaa kumtwaa Falcao
    War: Sir Alex Ferguson is set to rival Roberto Mancini for the Atletico Madrid sensation
    Vita: Sir Alex Ferguson amejipanga kupambana na Roberto Mancini kuwania saini ya kifaa cha Atletico Madrid

    Kocha wa Atletico, Diego Simeone amezungumzia tetesi hizo kwa kusema: "Falcao ni mchezaji mkubwa na dhahiri timu kubwa duniani zinamuhitaji. Hainishangazi.".
    Ikiwa United itampata Falcao litakuwa ni pigo zaidi kuwa Chelsea, ambao inafikiriwa walishinda mbio za kumsaini, na kocha wa City, Roberto Mancini ambaye anaamini uamuzi wa Robin van Persie kuhamia Old Trafford badala ya Etihad imekuwa sababu kubwa ya matokeo ya msimu huu. 
    Pamoja na hayo, klabu yoyote inayotaka kumsaini Falcao italazimika kumaliza pia na wamiliki wengine wawili, kutokana na ukweli kwamba, kampuni inayoendeshwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa zamani wa United na Chelsea, Peter Kenyon na wakala Jorge Mendes wana hisa kwa mchezaji huyo tangu wasaidie dau la Pauni Milioni 34 katika uhamisho wake kutoka Porto.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIR ALEX FERGUSON APIGA HATUA KUBWA KATIKA KUWANIA SAINI YA MKALI WA MABAO RADAMEL FALCAO ANAYEZITOA UDENDA MAN CITY NA CHELSEA PIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top