• HABARI MPYA

    Sunday, April 14, 2013

    MAMBO YALIVYOKUWA SIMBA NA AZAM FC TAIFA LEO

    Wamesujudu: Wacheza wa Simba SC wakiwa wamesujudu baada ya kupata bao la pili katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC, jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya 2-2, baada ya Simba SC kuongoza 2-0 hadi mapumziko.

    Kocha Msaidizi wa Azam FC, aliiongoza timu leo baada ya bosi wake, Muingereza mwenzake, Stewart Hall kutolewa nje kipindi cha kwanza kwa kutoa lugha chafu

    Shomary Kapombe wa Simba (kushoto) akimiliki mpira mbele ya beki wa Azam FC, David Mwantika

    Kipre Tchetche wa Azam akiwania mpira mbele ya beki wa Simba SC, Miraj Adam

    Mrisho Ngassa wa Simba SC (kulia) akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Azam FC, David Mwantika

    Kipa wa Simba SC, Abbel Dhaira akiwa amedaka mpira wa juu

    David Mwantika wa Azam akiondosha mpira miguuni mwa Shomary Kapombe

    Wachezaji wa Simba na Azam wakigombea mpira wa juu

    Salum Abubakar 'Sure Boy'  wa Azam FC, akiondoka na mpira pembeni ya kiungo wa Simba SC, Amri Kiemba 

    Mwadini Ally, kipa wa Azam akiwa amejishika kiuno baada ya kufungwa bao la pili 

    Wachezaji wa Simba SC wakishangilia bao la pili mbele ya jukwaa la mashabiki wao

    John Bocco wa Azam amefumua shuti mbele ya mabeki wa Simba SC

    Mussa Mudde wa Simba SC kulia akimiliki mpira pembeni ya john Bocco wa Azam

    John Bocco akituliza mpira kwa kifua...

    Himid Mao wa Azam kushoto akimiliki mpira pembeni ya Amri Kiemba wa Simba SC

    11 wa Simba SC walioanza leo

    Wa benchi; Kutoka kulia kocha Patrick Liewig, Juma Kaseja, bFelix Sunzu, Mwinyi Kazimoto na Edward Christopher

    11 wa Azam walioanza leo

    Kocha Msaidizi wa Simba SC, Jamhuri Kihwelo akilalamika jambo kwa refa wa akiba, Israel Nkongo

    Mashabiki wa Yanga walikuwepo Taifa leo kuishangilia SImba SC

    Kipre Tchetche amelala chini kupiga mpira dhidi ya Shomary Kapombe

    Kipre Tchetche akimkimbia Shomary Kapombe...

    Mfungaji wa mabao ya Simba SC leo, Ramadhani Singano 'Messi'

    John Bocco anapasua...

    Bao: Kipa wa Simba SC, Abbel Dhaira akichupa kulia, mpira ukienda kushoto kwake kufuatia mkwaju wa penalti wa Kipre Tchetche

    Michezo ni furaha, si uadui; Mrisho Ngassa wa Simba SC akifurahia na Himid Mao wa Azam baada ya mechi. Kushoto kabisa ni Kocha wa Viungo wa Azam, Ibrahim Shikanda

    Kipre Tchetche akiokota mpira kwenye nyavu za Simba pembeni ya kipa Abbel Dhaira baada ya kufunga penalti

    Kocha Stewart Hall akimsemea mbovu refa Orden Mbaga, jambo lililomponza kutolewa uwanjani 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MAMBO YALIVYOKUWA SIMBA NA AZAM FC TAIFA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top