• HABARI MPYA

    Tuesday, April 09, 2013

    BALOTELLI AFUNGIWA MECHI TATU ITALIA KWA KUMBWATUKIA MSHIKA KIBENDERA JUMAPILI


    MSHAMBULIAJI wa AC Milan, Mario Balotelli amefungiwa mechi tatu za Serie A baada ya kumbwatukia mshika kibendera katika mechi dhidi ya Fiorentina juzi.
    Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City, Balotelli tayari alikuwa amefungiwa moja kwa moja mechi moja baada ya kupata kadi yake ya nne ya njano msimu huu katika mechi hyo iliyoisha kwa sare ya 2-2.
    Calm down: Fiorentina keeper Emiliano Viviano (centre) embraces Balotelli, arguing with linesman Daniele Doveri
    Tulia wewe: Kipa wa Fiorentina, Emiliano Viviano (katikati) akimtuliza Balotelli, wakati anamtupia maneno mshika kibendera Daniele Doveri
    Balotelli
    Balotelli
    Hata hivyo akaongezewa adhabu ya mechi mbili zaidi katika taarifa iliyotolewa leo kwa kosa la kumbwatukia mshika kibendera huyo.
    Mshambuliaji huyo wa Italia ameifungia mabao 10 klabu na timu yake ya taifa katika mechi 11 mwaka huu, lakini atakosa mechi zijazo za Milan dhidi ya Napoli na Juventus sambamba na Catania.
    In action: Balotelli played up front for Milan in the 2-2 draw, seen here going up for a high ball
    Kazini: Balotelli alisimama mbele wakati Milan inatoa sare ya 2-2, angalia hapa anavyochukua mpira wa juu
    balotelli
    Balotelli akipambana

    Milan inashika nafasi ya tatu Serie A, ikizidiwa pointi nne na Napoli katika kinyang'anyiro cha nafasi ya pili, huku Juventus ikiongoza kwa poinyi tisa zaidi.
    Tukio hilo linakuja mara tu baada ya Balotelli kukutwa anavuta sigara chooni kwenye treni.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BALOTELLI AFUNGIWA MECHI TATU ITALIA KWA KUMBWATUKIA MSHIKA KIBENDERA JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top