• HABARI MPYA

    Wednesday, April 10, 2013

    ARSHAVIN KUTUNGIKA DALUGA MWISHONI MWA MSIMU


    KIUNGO wa Arsenal, Andrey Arshavin anaweza kustaafu soka mwishoni mwa msimu wakati mkataba wake utakapomalizika Uwanja wa Emirates.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, tayari ameambiwa hatapewa mkataba mpya baada ya kushindwa vita ya namba katika kikosi cha kwanza cha Arsene Wenger.
    Kwa maana hiyo, mchezaji anayeshikilia rekodi ya kusajiliwa kwa bei mbaya Arsenal, atatungika daluga zake licha ya taarifa kwamba anatakiwa na klabu kadhaa China na Marekani.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Urusi, amecheza mechi saba tu za Ligi Kuu na Washika Bunduki hao msimu huu, baada ya msimu uliopita kupelekwa kwa mkopo Zenit ya nyumbani kwao.
    Ready to retire: The Russian international is considering ending his playing career in the summer
    Tayari kustaafu: Kiungo wa kimataifa wa Urusi, anatarajiwa kustaafu mwishoni mwa msimu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ARSHAVIN KUTUNGIKA DALUGA MWISHONI MWA MSIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top