• HABARI MPYA

    Monday, March 11, 2013

    BADO NIPO NIPO SANA SIMBA SC, ASEMA DK KAPINGA

    Cossmas Kapinga wa kwanza kulia akiwa na kocha wa makipa, James Kisaka, Moses Basena na Jamhuri Kihwelo.

    Na Princess Asia
    DAKTARI wa Simba SC, Cossmas Kapinga amesema hajaacha kazi katika klabu hiyo na kutokuwepo kwake kazini kwa sasa kunatokana na ruhusa maalum ya uongozi, kwa shughuli nyingine za kijamii.
    Dk. Kapinga ameiambia BIN ZUBEIRY mida hii kwamba, ameomba ruhusa kwa uongozi na taarifa zake anazo Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala.
    Amesema amechukuliwa na shirika la Kimarekani la Engender Health kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwenda kutoa mafundisho kwa madaktari juu ya namna kutoa huduma ya uzazi wa mpango wilayani Masasi mkoani Mtwara.
    Amesema zoezi hilo linaanza leo Machi 11 na linatarajiwa kufikia tamati Machi 22, mwaka huu.
    Kutokana na kutoonekana jana uwanjani wakati Simba SC ikimenyana na Coastal Union ya Tanga, ikadaiwa Kapinga naye amejiuzulu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BADO NIPO NIPO SANA SIMBA SC, ASEMA DK KAPINGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top