• HABARI MPYA

    Saturday, March 30, 2013

    MANA CITY, ARSENAL, SPURS ZAUA ENGLAND, CHELSEA CHALIIIII


    KLABU ya Arsenal imeongeza matumaini ya kucheza Ligi ya mabingwa kufuatia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Reading kwenye Uwanja wa Emirates, ambao unawapeleka The Royals mkiani mwa Ligi Kuu England.
    Katika mchezo huo, mabao ya Arsenal yalifungwa na Gervinho dakika ya 11, Cazorla dakika ya 48, Giroud dakika ya 67 na Arteta dakika ya 77, wakati bao pekee la kufutia machozi la Reading lilifungwa na Robson-Kanu dakika ya 68.
    Katika mchezo huo, kikosi cha Arsenal kilikuwa; Fabianski, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Monreal/Gibbs dk71, Arteta, Rosicky, Ramsey, Gervinho/Oxlade-Chamberlain dk75, Cazorla na Giroud/Podolski dk75.
    Reading: Taylor, Kelly, Pearce, Mariappa, Shorey, Leigertwood, Karacan/Akpan dk76), Guthrie, McAnuff, Robson-Kanu/McCleary dk80) na Pogrebnyak/Hunt dk61.
    Three points: Bacary Sagna congratulates Gervinho after smashing home Arsenal's first
    Pointi tatu: Bacary Sagna akimpongeza Gervinho baada ya kuifungia Arsenal bao la kwanza

    Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, Chelsea ililala 2-1 mbele ya Southampton kwenye Uwanja wa St Mary's, mabao ya washindi yakitiwa kimiani na Rodriguez dakika ya 23 na Lambert dakika ya 35, wakati la kufutia machozi la The  Blues likifungwa na John Terry dakika ya 33.
    Kikosi cha Chelsea kilikuwa;Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Terry, Bertrand, Mikel/Ramires dk71, Lampard, Moses, Oscar/Benayoun dk76, Marin/Hazard dk60 na Torres.  
    Southampton: Boruc/Kelvin Davis dk46, Clyne, Yoshida, Hooiveld, Shaw, Puncheon/Ward-Prowse dk62, Schneiderlin, Cork, Steven Davis/Fox dk85, Rodriguez na Lambert.
    Dejection: Chelsea's top-four hopes suffered a major blow as they were beaten 2-1 on the south coast
    Pigo: Wachezaji wa Chelsea wakiwa hoi baada ya kipigo
    Tottenham Hotspur imeshinda 2-1 dhidi ya Swansea, mabao yake yakitiwa kimiani na Vertonghen dakika ya saba na Bale dakika ya 21, wakati la wapinzani wao lilifungwa na Michu dakika ya 71.
    Gareth Bale (R) scores Tottenham's second goal
    Gareth Bale (kulia) akiifungia Tottenham bao la pili

    West Ham United imeshinda 3-1 dhidi ya West Bromeich, mabao yake yakitiwa kimiani na Carroll dakika ya 16 na 80 na O'Neil dakika ya 28, wakati la kufutia machozi la wapinzani wao lilifungwa na Dorrans dakika ya 88 kwa penalti.
    Happy Hammers: West Ham players celebrate Carrol's early effort
    Shangwe za ushindi: Wachezaji wa West Ham wakimpongeza Carrol baada ya kufunga bao la pili 

    Manchester City imeshinda 4-0 dhidi ya Newcastle, mabao yake yakifungwa na Carlos Tevez dakika ya 41, David Silva dakika ya 45, Nahodha wake, Vincent Kompany dakika ya 56 na Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure dakika ya 59. 
    One's Kompany: Manchester City captain Vincent Kompany celebrates his goal
    Asante Kompany: Nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany akipongezwa na wenzake kwa kufunga
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MANA CITY, ARSENAL, SPURS ZAUA ENGLAND, CHELSEA CHALIIIII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top