• HABARI MPYA

  Monday, March 25, 2013

  WA STARS YANGA WAPEWA 'OFF' MBILI

  Baadhi ya wachezaji wa Yanga;kutoka kulia Haruna Niyonzima, Nadir Haroub 'Cannavaro', Athumani Iddi 'Chuji' na Oscar Joshua.

  Na Mahmoud Zubeiry
  WACHEZAJI watano wa klabu ya Yanga SC, waliokuwa katika kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wamepewa mapumziko ya siku mbili na kocha wao, Ernie Brandts baada ya mechi ya jana na Morocco.
  Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, wachezaji hao Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Frank Domayo, Athumani Iddi ‘Chuji’ na Simon Msuva wataungana na wenzao Jumatano.
  Wachezaji wengine wote wa Yanga wanaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Polisi mjini Morogoro mwishoni mwa wiki.
  Wengine wanaokosekana Yanga kwa sasa ni beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima waliokuwa na timu ya taifa ya Rwanda na mshambuliaji Hamisi Kiiza aliyekuwa na timu ya taifa ya Uganda kwa mechi za kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia mwishoni mwa wiki. 
  Kizuguto alisema zaidi ya hao, mwingine anayekosekana ni beki Ladislaus Mbogo ambaye amepewa mapumziko maalum baada ya kufanyiwa upasuaji wa shavu.
  Yanga imeshika kasi katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu, ikiwa inaongoza kwa pointi zake 48, ikifuatiawa na Azam FC yenye pointi 37 na mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 34.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: WA STARS YANGA WAPEWA 'OFF' MBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top