• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 24, 2013

  STARS WALIVYOICHANA CHANA MOROCCO TAIFA LEO, ULIMWENGU ALIKUWA NOMA LEO

  Mshambuliaji wa Tanzania, Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Morocco,  Issam Eladoua katika mchezo wa Kundi C kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil mwakani uliofanyika jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Taifa Stars ilishinda mabao 3-1.

  Hatari kwenye lango la Morocco

  Bao la tatu; Samatta akikimbia kushangilia baada ya kufunga bao la tatu, huku kipa wa Morocoo, Nadir Lamyaghri akijikokota chini baada ya jithada zake za kuokoa kushindwa na mpira umenasa kwenye nyavu

  Mrisho Ngassa akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Morocco, AbderrahimAchchakir

  Shuti la bao; Thomas Ulimwengu akiwa amefumua shuti kufunga bao la kwanza

  Wachezaji wa Stars wakimpongeza Ulimwengu kufunga bao lililofungua biashara  nzuri leo

  Mrisho Ngassa akipasua katikati ya mabeki wa Morocco

  Mpira nyavuni; Bao la kwanza lililofungwa na Ulimwengu

  Beki wa Morocco, Younes Hammal akiondosha hatarini langoni mwake mbele ya wachezaji wa Stars, Amri Kiemba na Mrisho Ngassa kushoto

  Shuti; Mwinyi Kazimoto angekuwa wa kwanza kuifungia Stars leo kama shuti lake hili lisingeokolewa na mabeki wa Morocco

  Wachezaji wa Stars wakimpongeza Samatta aliyefunga bao la pili

  Hatari kwenye lango la Morocco

  Thomas Ulimwengu akiwatoka mabeki wa Morocco

  Ulimwengu anakwenda chini baada ya kukwatuliwa na beki wa Morcco  nyuma...jamaa alimkwatua Uli na mchezaji mwenzake huyo mbele kwa pamoja ambaye alikuwa anamsindikiza Thom 

  Sura za huzuni; Wachezaji wa akiba wa Morocco walishindwa kuendelea na mazoezi ya kupasha misuli moto  na kubaki wanastaajabu namna vijana wa Tanzania wanavyowatesa wenzao uwanjani 

  Thomas Ulimwengu akimfunga tela beki wa Morocco, Abderrahim Achchakir

  Kikosi cha Morocco leo

  Utabiri huu bado kidogo utimie leo; Mashabiki wakiwa na bango linaloonyesha Taifa Stars 3-0 Morocco

  11 wa Stars walioanza leo

  Bao la tatu; Wachezaji wa Stars wakimpongeza Samatta baada ya kufunga bao la tatu

  Katika picha ndogo kushoto, Thomas Ulimwengu ndio ampitishia kanzu Abderrahim Achchakir na picha kubwa tayari kanzu imemtosha mtu...

  Ulimwengu anapasua katikati ya mabeki wa Morocco..leo jamaa katufaa sana Watanzania

  Mbwana Samatta anapiga shuti

  Beki nwa Morocco, Zakarya Bergdich akijaribu kuupitia mpira miguuni mwa beki wa Stars, Erasto Nyoni

  Beki wa Morocco, Abdelillah Hafidi akimkanyaga kiungo wa Stars, Amri Kiemba kwenye eneo la hatari...

  Kiemba kaenda chini...lakini refa alipitiwa hapa kibinadamu akapeta

  Beki wa Stars, Shomary Kapombe akipasua katikati ya wachezaji wa Morocco

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: STARS WALIVYOICHANA CHANA MOROCCO TAIFA LEO, ULIMWENGU ALIKUWA NOMA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top