• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 30, 2013

  KAGERA SUGAR WAISHUSHIA MBALI SIMBA SC LIGI KUU

  Kagera Sugar; Wameishusha Simba SC

                            P W D L GF GA GD Pts
  1 Yanga 21 15 4 2 37 12 25 49
  2 Azam 21 13 4 4 36 16 20 43
  3 Kagera Sugar 22 10 7 5 24 18 6 37
  4 Simba SC 21 9 8 4 30 19 11 35
  5 Coastal Union 22 8 8 6 23 20 3 32
  6 Mtibwa Sugar 22 8 8 6 24 21 3 32
  7 Ruvu Shooting 20 8 5 7 21 19 2 29
  8 JKT Oljoro 22 7 7 8 22 23  -1 28
  9 Mgambo JKT    21 7 3 11 15 21 -6 24
  10 JKT Ruvu 21 6 4 11 19 34 -15  22
  11 Prisons 21 4 8 9 11 20 -9 20
  12 African Lyon 22 5 4 13 15 32 -17 19
  13 Polisi Moro 22 3 8 11 12 22 -10 18
  14 Toto African 22 3 9 10 19 31 -12 18

  Na Prince Akbar
  KAGERA Sugar imeishusha Simba SC hadi nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 nyumbani dhidi ya ndugu zao, Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba jioni hii.
  Ushindi huo, unaifanya Kagera inayofundishwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Abdallah ‘King’ Kibadeni kutimiza pointi 37 baada ya kucheza mechi 22.
  Katika mchezo huo, mabao ya Kagera yalifungwa na Maregesi Mwangwa dakika ya 35 na Themis Felix dakika ya 67, wakati na kufutia machozi la Mtibwa lilifungwa na Vincent Barnabas dakika ya 50.
  Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, JKT Oljoro iliutumia vyema Uwanja wa nyumbani, Sheikh Amri Abeid mjini Arusha baada ya kuichapa JKT Ruvu mabao 2-0.
  Mabao ya Oljoro yalifungwa na Iddi Swaleh dakika ya nne na Paul Nonga dakika ya nane.
  African Lyon ilifanikiwa kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jioni hii, bao pekee la Adam Kingwande dakika ya 47.
  Lyon sasa imejitoa mkiani hadi hadi nafasi ya 12 juu ya Polisi na Toto, baada ya kutimiza pointi 19 ikizizidi kwa pointi moja timu hizo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: KAGERA SUGAR WAISHUSHIA MBALI SIMBA SC LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top