• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 19, 2013

  RONALDO ASHINDA TUZO MCHEZAJI BORA HISPANIA ILA KUBAKI REAL...

  NYOTA Cristiano Ronaldo jana alizawadiwa tuzo ya Alfredo Di Stefano kwa kuwa Mchezaji Bora msimu uliopita wa La Liga, lakini hata hivyo akagoma kuthibitisha kama atabaki Real Madrid.
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ureno alikuwa tegemeo la Real wakati wakiwafunga wapinzani wao Barcelona kutwaa taji lao la kwanza la ligi tangu mwaka 2008 na mbele ya wengi anaonekana kama miongoni mwa wachezaji bora duniani.
  Lakini kama ilivyo kwa kocha Jose Mourinho anataka kuondoka mwishoni mwa msimu, akifikiriwa kutimkia ama Manchester United au Paris Saint-Germain, kuna shaka mchezaji huyo ataondoka na mwalimu wake.
  Ukweli ni kwamba Ronaldo, hakujadili mustakabali wake katika klabu baada ya kukabidhiwa tuzo na Di Stefano mwenyewe.
  Outstanding: But Cristiano Ronaldo may not be remembered with the same fondness as Di Stefano
  Cristiano Ronaldo akikabidhiwa tuzo na Di Stefano
  Past and present: Di Stefano and Ronaldo came face to face
  Di Stefano alipokutana uso kwa uso na Ronaldo
  La Liga's best? Ronaldo was awarded the trophy based on his efforts in the 2011/2012 season
  Bora La Liga? Ronaldo alizawadiwa tuzo hiyo kutokana na mchango wake wa msimu wa 2011/2012

  WAKALI KWELI: ALFREDO DI STEFANO V CRISTIANO RONALDO

  Alfredo Di Stefano
  Alfredo Di Stefano
  Kuzaliwa: Julai 4, 1926
  Alipozaliwa: Buenos Aires (Argentina)
  Nafasi: Mshambuliaji
  Klabu: River Plate (1945, 1947-49 ), Huracán (1946), Millonarios (1949-52), Real Madrid (1953-64), Espanyol (1964-66).
  Timu ya taifa: Mechi 31 (Mabao 23) akiwa na Hispania; Mechi 6 (Mabao 6) na Argentina
  HESHIMA, MATAJI:
  5 Kombe la Ulaya (Real Madrid, 1956, 1957, 1958, 1959, 1960)
  1  Kombe la Mabara (Real Madrid, 1960)
  1  Kombe la America (River Plate, 1947)
  8 Ligi ya Hispania (Real Madrid, 1954, 1955, 1957, 1958, 1961, 1962, 1963, 1964)
  1 Kombe la Hispania (Real Madrid, 1962)
  2 Ligi ya Argentina (River Plate, 1945, 1947)
  4 Ligi ya Colombia (Millonarios Bogotá, 1949, 1951, 1952, 1953)
  La Liga's best? Ronaldo was awarded the trophy based on his efforts in the 2011/2012 season
  Cristiano Ronaldo
  KUzaliwa: Februari 5, 1985
  AlipozaliwaFunchal, Madeira (Ureno)
  Nafasi: Mshambuliaji
  Klabu: Sporting Lisbon (2001-2003), Manchester United (2003-2009), Real Madrid (2009 hadi sasa).
  Timu ya taifa: Mechi 101 (Mabao 38) na Ureno

  HESHIMA, MATAJI:
  1 Kombe la Ulaya (Manchester United, 2008)
  3 Ligi Kuu England (Manchester United, 2007, 2008, 2009)        1 Kombe la FA (Manchester United, 2004)                                            1 Kombe la Ligi (Manchester United, 2006)                                                                                           1 Ligi ya Hispania (Real Madrid, 2012)                                                                                               1 Kombe la Hispania (Real Madrid, 2011)
  1 Super Cup ya Hispania (Real Madrid, 2012)                                                                                          1 Ligi ya Ureno (Sporting Lisbon, 2002                                                                                     1 Super Cup ya Ureno (Sporting Lisbon, 2002)                                                                              1 Kombe la Ureno (Sporting Lisbon, 2002)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: RONALDO ASHINDA TUZO MCHEZAJI BORA HISPANIA ILA KUBAKI REAL... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top