• HABARI MPYA

    Friday, March 29, 2013

    KOMPANY ANUNUA KLABU UBELGIJI, ANATAKA KUIBADILI JINA IWE TISHIO ULAYA


    AKIWA bado mchezaji wa Manchester City inayopambana kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu England, beki Vincent Kompany ameamua kununua klabu inayosuasua katika Ligi Daraja la Tatu Ubelgiji, FC Bleid.
    Ikiwa imeshinda mechi mbili tu katika ya 28 ilizocheza D3B msimu huu, klabu hiyo kutoka Jiji la Brussels iko mkiani mwa Ligi na ina deni la pointi 16 ili kuwa salama, lakini Kompany anaamua kuwekeza huku akiendelea kucheza.
    Katika taarifa iliyobandikwa katika tofuti mpya ya klabu hiyo, WeStartFromScratch.commchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameelezea sababu zake za kuinunua timu hiyo kuwekeza ili irejeshe makali yake na kuwa tishio Ulaya.
    Patriot: Kompany, seen here with Mousa Dembele (right) has never been shy of his love for his country
    Kombora: Kompany, anaonekana hapa akiwa na Mousa Dembele (kulia), hajawahi kuona aibu kuonyesha mapenzi yake kwa nchi yake.

    Na Kompany anawakaribisha wadau wa soka, awe shabiki au asiwe shabiki wa klabu hiyo, kujitokeza kusaidia mawazo ya kupatikana kwa jina jipya la klabu hiyo.
    Get involved: Kompany has urged anyone to get involved and suggest a new name for the club
    Karibu: Kompany amemkaribisha yeyote kuchangia wazo la jina jipya la klabu
    Kompany, ambaye amekulia Brussels, amesema: "Ni mchezo wangu na jukumu la kijamii la kuwaunganisha vijana wa Brussels.
    Vijana wa Brussels, kutoka sehemu tofauti, wanang'ara na wanajiamini mno, lakini hawapewi nafasi.
    "Mimi ni miongoni mwao na ninamini kwa jitihada hizi katika eneo sahihi, wanaweza chochote... kama watapewa nafasi,"alisema beki huyo.
    Beki huyo hayuko peke yake katika uwekezaji huo, na anasema ataendelea kuzingatia ajira yake  Eastlands na majukumu yake katika timu ya taifa ya Ubelgiji.
    Back on their feet: The Brussels-born defender (bottom) wants to give something back to the City and revitalise the club
    Furaha na timu ya taifa: Beki mzaliwa wa Brussels (chini kabisa) anataka kulipa fadhila nyumbani kwao kwa kuwekeza katika klabu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KOMPANY ANUNUA KLABU UBELGIJI, ANATAKA KUIBADILI JINA IWE TISHIO ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top