• HABARI MPYA

    Tuesday, March 26, 2013

    RASHARASHA ZAANZA MISS TABATA 2013


    Washiriki wa Miss Tabata 2013 wakipozi mazoezini Da West Park, Tabata
    Na Princess Asia
    JUMLA ya warembo 23 wamejitokeza kushiriki katika shindano la kumtafuta Miss Tabata 2013 ambalo litazinduliwa siku ya Pasaka kwenye ukumbi wa Da’ West Park Tabata.
    Mratibu wa shindano hilo, Godfrey Kalinga alisema jana warembo hao watatambulishwa pamoja na wale wanaoshiriki Miss Mzizima siku ya sikukuu ya Pasaka Da West Park.
    Kalinga aliwataja warembo waliojitokeza kuwania taji la Miss Tabata 2013 na kuendelea na mazoezi Da West Park ni Martha Gewe (19), Zilpha Christopher (19), Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19), Amina Ally (18), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19),  Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20), Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).
    Aliwataja wengine ni Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rachel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Blath Chambia (23), Ray Issa (22), Shamim Abass (22) na Shan Abass (22).
    Utambulisho wa warembo hao, utasindikizwa na burudani kabambe kutoka bendi ya Twanga Pepeta “Wazee wa Kisigino”.
    Kapinga alisema wapenzi wa tasnia ya urembo Jijini Dar es Salaam, watapata fursa ya kuwaona warembo kabla ya Miss Tabata kufanyika Mei mwaka huu.
    Miss Tabata 2013 imedhaminiwa na Konyagi, CXC Africa, Fredito Entertainment na Saluti5 na kuandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.
    Washindi watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki Miss Ilala baadaye mwaka huu.
    Anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: RASHARASHA ZAANZA MISS TABATA 2013 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top