• HABARI MPYA

    Thursday, March 28, 2013

    SUAREZ HATARINI KUFUNGIWA NA FIFA KWA KUMCHAPA KONDE MCHEZAJI WA CHILE


    FIFA itaamua kumuadhibu au la Luis Suarez mara itakapopata ripoti ya refa aliyechezesha mechi kati ya Uruguay na Chile kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
    Mshambuliaji huyo wa Liverpool alinaswa na kamera za Televsheni akimrupia konde mchezaji wa Chile, Gonzalo Jara, lakini Nestor Pitana, Ofisa wa mechi hakulinukuu tukio hilo, baada ya kuzungumza na wawili hao kufuatia kuvurugana kwao wakati wa kona.
    Ikiwa itabainika ni kweli alifanya hivyo, Suarez atakuwana na rungu la FIFA ingawa haiwezi kufanya hivyo hadi ipate ripoti rasmi ya refa ya maandishi.
    Incident: Luis Suarez hit Gonzalo Jara in the face
    Tukio: Luis Suarez akimchapa konde Gonzalo Jara usoni.
    Banned: Suarez will already serve a suspension for accumulated yellow cards
    Kifungoni: Suarez tayari atatumikia adhabu ya kadi za njano.

    Msemaji wa FIFA amesema: "Tutaendelea kukusanya ripoti zote za mechi, kwa kuwa marefa wana saa 24 ya kuwasilisha ripoti hizo. Tutaangalia kilichomo kwenye ripoti zao, kisha FIFA itachukua hatua kwa mujibu wa ripoti hizo."
    Suarez tayari anakabiliwa na adhabu ya kusimamishwa baada ya kupewa kadi ya njano dakika za lala salama katika medhi dhidi ya Chile kwa utovu wa nidhamu. 
    Atakosa mechi ijayo ya Urugay dhidi ya Venezuela mwezi Juni kuwania Fainali za Brazil, ambayo ni habari njema kwa klabu yake Liverpool.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SUAREZ HATARINI KUFUNGIWA NA FIFA KWA KUMCHAPA KONDE MCHEZAJI WA CHILE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top