• HABARI MPYA

    Wednesday, March 20, 2013

    GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE MAMBO YAANZA LEO

    Washiriki

    Na Princess Asia
    WAKATI umewadia tena wa kushuhudia mapambano katika kipindi ukipendacho cha Televisheni na kinachotambulika  kama, “The GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™”, ambacho kinarudi kwenye runinga yako  wiki hiii tarehe 20 mwezi huu wa tatu.  
    Mwaka huu watazamaji watapata nafasi ya kuangalia mchuano huu wa kipindi hiki katika televisheni mbili  ikiwemo televisheni ya ITV na Clouds TV ambazo zitarusha kipindi hiki kwa muda tofauti tofauti siku hiyo ya Jumatano.
    Ikumbukwe kwamba  mamia ya vijana kutoka kona mbali mbali nchini walichuana vikali hapo leaders  club ambapo walikua na nafasi ya kuweza kuingia kwenye shindano ambalo lingewawezesha kujishidia kitita cha dola za kimarekani $250,000.  Kipindi hiki cha televisheni kinachotazamwa na wengi barani Afrika kimerudi tena kwa kishindo na kwa sasa kitakuwa kinashirikisha nchi za barani Africa.  Washiriki watakuwa kutoka nchi za Cameroun, Ghana, Kenya, Tanzania and Uganda na washindi wa mwisho kabisa watajipatia tuzo ya  ‘Pan-African champions.’
    Washiriki wote watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kwamba wanaweza kuwakilisha  nchi zao ipasavyo .  GUINNESS  ilipigania kutafuta kwa hali ya juu washiriki walio na uwezo mkubwa na waliokuwa tayari kuonyesha vipaji vyao na ujasiri kwenye mchezo wa soka.   Timu zote zitashiriki kwa vipaji na kwa uelewa wa soka yaani kwa kiingereza, ‘Skill and Knowledge’ .  Kwa hivyo kila timu ina washiriki wawili.  Mmoja kwa maswala ya uelewa na mwingine kwa suala zima la kipaji. 
    Kwa kuanza kabisa, watanzania waliofuzu kusafiri watakutanishwa wenyewe kwa wenyewe jukwaani, na kupewa maswali na nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwenye soka.  Baada ya hapo watakaothibitisha kuwa wapo juu zaidi kwa asilimia mia, watapata nafasi ya kuingia kwenye shindano lenyewe wakipewa dhamana ya kubeba bendera ya nchi yao. Wengine watarudi nyumbani.
    Usikose kipindi cha kwanza kabisa ambacho kitarushwa hewani na televisheni ya ITV saa tatu na dakika kumi na tano usiku na Clouds TV  saa mbili na dakika kumi na tano usiku siku  ya jumatano  tarehe 20 machi mwaka huu.  Katika kipindi hiki, tutapata nafasi ya kushuhudia  timu yetu  ikichuana vikali katika raundi ya kwanza. 
    Timu kwenye raundi ya kwanza:

    Timu ya bluu – Tanzania:
    Kutoka Dar es Salaam, Daniel Msekwa,  ndiye kiongozi kwenye maswala ya maswali yanayohusiana na soka,  Mwalimu Akida Hamad, naye ataonyesha kipaji kwa kucheza .  Daniel ni mfanyakazi wa shirika la bandari Tanzania yaani TPA na Mwalimu bado ni mwanafunzi wa chuo cha elimu ya juu.  Wote wanakubali kwamba mchezo huu umewapa nafasi vijana wengi kuonyesha vipaji vyao na kwamba unainua soka sio kwa kucheza tu bali na kuwa na uelewa kuhusu mchezo mwenyewe.  Je wataweza kuendelea kwenye hatua ya pili?

    Timu Nyekundu – Kenya:
    Hawa wapenzi wa michezo mmoja ni Michael Kirwa,  na mwenzake ni mwalimu wa mazoezi  yaani ‘fitness trainer’ Stephen Githinji, wote wa jiji la Nairobi.  Michael yupo hapa kwa maswala ya kujibu maswali yani uelewa wa soka naye Stephen ndiye atakayeonyesha vipaji kwa kucheza .

    Timu ya kijani – Uganda:
    Oscar Boban na  Kennedy Andindu, wanatokea kampala na ndio watakaoakilisha Uganda katika hiki kipindi cha kwanza.  Oscar ni mfanyabiashara na ndiye atakayekuwa mshiriki wa uelewa na kennedy ambaye ni mpenzi wa Arsenal .Yeye atakuwa jukwaani kuonyesha kipaji chake. 

    Timu Nyeusi – Kenya: 
    Daniel Muthendu,  ni mhasibu na amekili ni mpenzi mkubwa wa soka na kujiamini kuchuana kwenye maswali yote yanayohusu mpira huu wa miguu.   Mwenzake ni Oscar Litonde,  ambaye ni mchezaji wa mpira, mechi za kirafiki jijini Nairobi.  Hawa nao pia watachuana vikali na timu tajwa hapo juu.

    Wapenzi wa kipindi hiki cha Guiness football challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba nao wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu.   Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili  bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi na kompyuta zao.   
    Pia GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook page www.facebook.com/guinnesskenya   Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kuupenda ukurasa huu yaani ‘like’ na utakuwa unapata habari zote kama zinavyotiririka.
    GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol iliyopo Afrika Kusini.  Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako. 
    Usisahau kuwa na kinywaji chako ukipendacho cha Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.  
    *Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane.  Tafadhali Kunywa kistarabu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE MAMBO YAANZA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top