• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 31, 2013

  SIMBA BILA NGASSA YATOA SARE NA SHINYANGA LEO

  Mrisho Ngassa; Hakucheza Shinyanga leo, alibaki Mwanza kusherehekea siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 23 leo

  Na Princess Asia
  BAADA ya jana kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na wenyeji Toto African kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni hii, Simba SC leo wametoa sare nyingine Shinyanga.
  Mabingwa hao wa Ligi Kuu ambao ni kama tayari wamekwishavuliwa taji hilo, wametoka sare ya kufungana bao 1-1 na Shinyanga United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga jioni ya leo.
  Simba ilicheza mechi hiyo, ili kuendelea kuwapa uzoefu wachezaji wake chipukizi, inaowatumia kwa sasa kwenye Ligi Kuu, baada ya kuwapiga chini baadhi ya nyota wa kikosi cha kwanza kwa utovu wa nidhamu.
  Miongoni mwa ‘mafaza’ waliotengwa ni Juma Nyosso, Haruna Moshi ‘Boban’, Amir Maftah, Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Komabil Keita, Abdallah Juma na Paul Ngalema.
  Katika mchezo wa leo, bao la Simba SC lilifungwa na Ramadhani Kipalamoto.
  Matokeo ya jana dhidi ya Toto, yanaifanya Simba SC iporomoke hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 35 baada ya kucheza mechi 21, nyuma ya Kagera Sugar yenye pointi 37, Azam pointi 43 na Yanga 49 kileleni. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SIMBA BILA NGASSA YATOA SARE NA SHINYANGA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top