• HABARI MPYA

    Friday, March 29, 2013

    HARUNA NIYONZIMA AREJEA DAR

    Yanga SC; Kuendeleza wimbi la ushindi kesho?


    Na Mahmoud Zubeiry
    KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima amerejea Dar es Salaam tangu jana akitokea Rwanda, alipokwenda kuitumikia timu yake ya taifa, Amavubi.
    Hata hivyo, Niyo hatakuwepo katika kikosi cha Yanga kitakachomenyana na Polisi Morogoro kesho Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
    Awali, jana Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto aliiambia BIN ZUBEIRY kwamba, Niyo alirejea na kuomba na ruhusa ya kurejea Rwanda kwa matatizo ya kifamilia, lakini leo ofisa huyo amesema kiungo huyo amerejea jana na yupo Dar es Salaam.
    Haruna yupo Dar

    MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
                               P W D L GF GA GD Pts
    1 Yanga 20 15 3 2 37 12 25 48
    2 Azam 20 12 4 4 35 16 19 40
    3 Simba SC 20 9 7 4 28 17 11 34
    4 Kagera Sugar 21 9 7 5 22 17 5 34
    5 Coastal Union 21 8 8 5 23 19 4 32
    6 Mtibwa Sugar  21 8 8 5 23 19 4 32
    7 Ruvu Shooting 19 8 5 6 21 18 3 29
    8 JKT Oljoro 21 6 7 8 20 23 -3 25
    9 Mgambo JKT 21 7 3 11 15 21 -6 24
    10 JKT Ruvu 20 6 4 10 19 32 -13 22
    11 Prisons 21 4 8 9 11 20 -9 20
    12 Polisi Moro  21 3 8 10 12 22 -10 17
    13 Toto African 21 3 8 10 17 29 -12 17
    14 African Lyon 21 4 4 13 14 32 -18 16


    Kizuguto alisema kikosi cha Yanga kimefanya mazoezi leo kwenye Uwanja wa Jamhuri tayari kwa mchezo wa kesho.
    Jana Kizuguto alisema wachezaji wengine wote wa kigeni wa Yanga wameenda na wenzao Morogoro tayari kwa mchezo huo wa kesho.  
    Hao ni beki Mbuyu Twite raia wa Rwanda pia na washambuliaji Hamisi Kiiza kutoka Uganda na Didier kavumbangu wa Burundi.
    Aidha, alisema kipa Said Mohamed aliumia mazoezini jana asubuhi naye hakwenda Morogoro. Kwa sababu hiyo, kipa aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili, Yanga B, Yussuf Abdul ndiye atakayekaa benchi kesho akimsikilizia Ally Mustafa ‘Barthez’.  
    Wachezaji wengine ambao hawakwenda Morogoro ni majeruhi Omega Seme, Salum Telela na Ladislaus Mbogo pamoja na chipukizi waliopandishwa kutoka B, Rehani Kibingu na George Banda.
    Yanga SC inaongoza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa pointi zake 48, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 40, Simba SC 34 sawa na Kagera Sugar.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: HARUNA NIYONZIMA AREJEA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top