• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 31, 2013

  SIMBA SC WATUA SHINYANGA KUSAFISHA NYOTA

  Yosso wa Simba; Watasafisha nyota Shinyanga leo?

  Na Princess Asia
  BAADA ya jana kulazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na wenyeji Toto African kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni hii, Simba SC leo watacheza mechi ya kirafiki Shinyanga.
  Mabingwa hao wa Ligi Kuu ambao ni kama tayari wamekwishavuliwa taji hilo, watashuka kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga jioni ya leo kumenyana na Shinyanga United.
  Mchezo huo, ni maaluma kwa Simba SC kuendelea kuwapa uzoefu wachezaji wake chipukizi, inaowatumia kwa sasa kwenye Ligi Kuu, baada ya kuwapiga chini baadhi ya nyota wa kikosi cha kwanza kwa utovu wa nidhamu.
  Miongoni mwa ‘mafaza’ waliotengwa ni Juma Nyosso, Haruna Moshi ‘Boban’, Amir Maftah, Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Komabil Keita, Abdallah Juma na Paul Ngalema.
  Matokeo ya jana dhidi ya Totot, yanaifanya Simba SC iporomoke hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 35 baada ya kucheza mechi 21, nyuma ya Kagera Sugar yenye pointi 37, Azam pointi 43 na Yanga 49 kileleni. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SIMBA SC WATUA SHINYANGA KUSAFISHA NYOTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top