• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 25, 2013

  TENGA KUFUNGUA SEMINA ELEKEZI COPA COCA COLA

  Tenga; Rais TFF

  Na Boniface Wambura
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa semina elekezi ya michuano ya Copa Coca Cola itakayofanyika kesho.
  Semina hiyo inayoshirikisha makatibu wakuu wa vyama vya mpira wa miguu mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na itafunguliwa na Rais Tenga kuanzia saa 3 kamili asubuhi.
  Washiriki wengine katika semina hiyo itakayokuwa na watoa mada kutoka TFF na wadhamini kampuni ya Coca Cola ni waratibu wa michuano ya Umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: TENGA KUFUNGUA SEMINA ELEKEZI COPA COCA COLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top