• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 29, 2013

  TOTO LA GEORGE WEAH LATUA CHELSEA, LAPANIA KUFANYA VITU VYA HATARI KULIKO BABA YAKE

  KLABU ya Chelsea imempa nafasi ya majaribio mtoto wa gwiji wa soka Liberia, mshambuliaji George Weah.
  Timmy, mwenye umri wa miaka 13, anataka kucheza London katika klabu ya zamani ya baba yake.
  Weah alijiunga na Chelsea kwa mkopo kutoka AC Milan mwaka 2000 na akafunga dhidi ya wapinzani Tottenham katika mchezo wake wa kwanza. Alikuwa mwenye furaha kupita kiasi kumpeleka mwanawe England kwa majaribio.
  Tribute: Weah, pictured with the FA Cup in 2000, had a message for his baby son on his shirt but then seemed to let the triumph go to his head (below)
  Weah, pichani akiwa na Kombe la FA mwaka 2000, alikuwa amebeba ujumbe kwa ajili ya mwanawe wa kiume katika fulana yake
  George Weah
  "Ana kipaji," Weah aliiambia talkSPORT. "Tunataka kumpa nafasi na pia tunataka afurahie mchezo ambao upo kwenye damu yake. Nimemleta Chelsea kwa ajili ya majaribio tu na kupata uzoefu tofauti."
  Alisema: "Wakati naondoka London, Niliendelea kuwa karibu na Chelsea na wakati kijana wangu anataka kuja England kucheza, mtu wa kwanza kumpigia ni baba yangu, Gary Staker [Ofisa wa klabu].
  On target: Weah only played for a short while at Chelsea but showed his nose for goal
  Amefunga: Weah alicheza muda  mfupi tu Chelsea, lakini alifanikiwa kufunga mabao ya kusisimua
  Strength of character: Weah was one of the world's greats at his peak
  Mtu wa nguvu: Weah alikuwa mmoja wa wachezaji wa kiwango cha juu duniani

  Angalau undugu huu wa kweli, tofauti...

  Ali Dia aliwasili Southampton mwaka 1996 na kudai ni mpwa wa Weah's (haikuwa kweli). Graeme Souness alicheza kamari na kumsajili. 
  Ulikuwa usajili wa aina yake - Souness alimuingiza katika mechi ya kwanza akitokea benchi, lakini akalazimika kumtoa nje dakika moja tu baadaye, kwani jamaa alikuwa mbovu ile mbaya. Na ndito akatemwa moja kwa moja.
  "Gary amefanikisha na Timothy anafurahia hii. Ameanza mazoezi tayari na anafurahia."
  Alipoulizwa juu ya hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari jana, kocha wa Chelsea, Rafa Benitez alionekana kutokuwa na uhakika juu ya Timmy, lakini Ofisa Habari akathibitisha hilo. 
  Timmy anataka kutengeneza njia yake mwenyewe katika soka na hataki kusafiria nyota ya baba yake.
  Alimuambia Tropigol: "Baba yangu alikuwa mmoja wa wanasoka baab kubwa duniani na ninataka kufuata nyayo zake.
  "Lakini pia ninataka kutengeneza jina langu mwenyewe. Nataka kuwa Timothy Weah, kuwa mimi mwenyewe, kucheza soka yangu na pia kufuata nyayo zake wakati nafanya hayo."
  Weah, aliyechezea pia Monaco, PSG na Man Citymbali na Chelsea na AC Milan, alishinda Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia mwaka 1995, na akachaguliwa pia Mwanasoka Bora wa karne wa Afrika. 
  At home: A few pictures of Weah at his apartment in west London in which he lived while he was at Chelsea
  Akiwa nyumbani: Picha chache za Weah katika mjengo wake wa hatari London aliokuwa anaishi wakati yupo Chelsea
  Sofa king
  Weah looking out of his window and on to the Thames
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: TOTO LA GEORGE WEAH LATUA CHELSEA, LAPANIA KUFANYA VITU VYA HATARI KULIKO BABA YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top