• HABARI MPYA

  Saturday, March 30, 2013

  MAN UNITED WAITWA NA BABA YAKE THIAGO WA BARCA WABEBE KIFAA


  KLABU ya Manchester United itaanza tena jitihada zake za kumsajili kiungo wa Barcelona, Thiago Alcantara baada ya baba yake kusema kijana wake huyo yuko tayari kuhama timu. 
  United imekuwa ikimmezea mate kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania kwa miaka mitatu sasa na ilitoa ofa ya Pauni Milioni 15 ambazo zilipigwa chini miezi 18 iliyopita. 
  Kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 sasa alipania kupambana kujihakikishia namba katika kikosi cha kwanza, lakini sasa amekubali yaishe na kuamua kuondoka.
  Wanted: Barcelona's Thiago Alcantara is a target for Manchester United
  Anatakiwa: Nyota wa Barcelona, Thiago Alcantara anatakiwa na Manchester United

  "Mwanangu anaweza kucheza vizuri zaidi katika timu nyingine yoyote duniani,:alisema baba yake, Mazinho. "Amejifunza mengi juu ya kucheza na wachezaji wakubwa, lakini Thiago ana malengo sana na anahitaji kucheza. 
  "Hakuna mmoja anayejua nini kitatokea katika mustakabali wake. Soka imebadilika sana na lolote linaweza kutokea. Kama Thiago anataka kwenda kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014, anahitaji kucheza zaidi.
  "Thiago ana kiwango cha kucheza Barca. Lakini atacheza zaidi katika klabu nyingine. Anaweza kujiunga na timu yoyote duniani.
  "Sijui kama Barca itanunua wachezaji zaidi mwishoni mwa msimu. Tayari wana wachezaji wengi sana ambao wanaweza kucheza kwenye kiungo. Pia, [kaka yake] Rafinha atakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza katika timu msimu ujao."
  Big fan: Sir Alex Ferguson will look to bolster his midfield in the summer
  Shabiki mkubwa: Sir Alex Ferguson ataangalia uwezekano wa kumsajili kiungo huyo mwishoni mwa msimu.

  Alcantara alitimkia Hispania akiwa ana umri wa miaka mitano na kusaini Barcelona miaka tisa baadaye.
  Alicheza mechi yake ya kwanza katika kikosi cha kwanza dhidi ya Mallorca mwaka 2009, na akafunga bao lake la kwanza mwaka uliofuata. Alisaini mkataba mpya miaka miwili iliyopita ambao alipunguziwa mshahara kutoka Euro Milioni 30 Pauni Milioni 25.
  Competition: Alcantara has been unable to force his way into the side
  Ushindani: Alcantara amekuwa mchezaji mshindani uwanjani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MAN UNITED WAITWA NA BABA YAKE THIAGO WA BARCA WABEBE KIFAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top