• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 17, 2013

  ZOLA WA YANGA KUZIKWA KESHO KISUTU, MSIBA UPO JANGWANI

  Hamza Said 'Zola' enzi
  za uhai wake

  Na Mwandishi Wetu
  ALIYEKUWA mhudumu wa klabu ya Yanga SC, Hamza Said maarufu kama Zola au Chiluba aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya gari, anatarajiwa kuzikwa kesho Saa 10:00 jioni katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
  Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kwamba kifo cha Hamza ni pigo kwa klabu, kwani alikuwa mchapakazi, mwaminifu na aliyejitolea mno kwa ajili ya klabu yake aipendayo.
  Alisema msiba upo makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani Dar es Salaam na ameomba wapenzi na wanachama kujitokeza kwa wingi kesho kumsindikiza mwenzao katika safari yake mwisho.
  Hamza alikutwa na umauti alfajiri ya leo, baada ya kugongwa na gari katika makutano ya Mitaa ya Rufiji na Kongo. Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: ZOLA WA YANGA KUZIKWA KESHO KISUTU, MSIBA UPO JANGWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top