• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 17, 2013

  MUSSA MGOSI BADO NOMA KWA MABAO, AIPIGIA MBILI JKT RUVU IKIIUA POLISI MORO

  Mussa Hassan Mgosi

  Na Prince Akbar
  JKT Ruvu ya Pwani, imejivuta kwa nafasi moja juu kutoka ya 11 hadi ya 10, kufuatia ushindi wa mabao 3-2 jioni hii dhidi ya Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Kwa matokeo hayo, JKT Ruvu inatimiza pointi 22, baada ya kucheza mechi 20, hivyo kuzidi kujiepusha na balaa la kushuka daraja.
  Mabao ya JKT leo yalitiwa kimiani na Mussa Hassan Mgosi katika dakika za 14 na 89 na Furaha Tembo dakika ya 32, wakati ya Polisi yalifungwa na Salum Machaku dakika ya 26 na Mokili Rambo kwa penalti dakika ya 45. 
  Polisi inabaki na pointi zake 17 katika nafasi ya 12 baada ya kucheza mechi 21, hivyo bado ipo kwenye hatari ya kurejea Daraja la Kwanza.
  Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mchezo mmoja kati ya African Lyon na JKT Oljoro Uwanja huo huo wa Azam. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MUSSA MGOSI BADO NOMA KWA MABAO, AIPIGIA MBILI JKT RUVU IKIIUA POLISI MORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top