• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 23, 2013

  CHRISTOPHER EDWARD AFUFUA MAKALI SIMBA SC

  Simba SC
  Na Princess Asia
  WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC leo wamelazimishwa sare ya kufungana na 1-1 na Rhino Rangers ya Tabora iliyopanda Ligi Kuu katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora, maalum kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba Jumatano, 
  Simba SC ambayo katika mchezo wake uliopita wa kirafiki iliifunga Singida United mabao 4-0, katika mchezo wa leo, bao lake limefungwa na Edward Christopher Shijja, mfungaji bora wa Kombe la BancABC Sup8R.
  Katika mchezo uliopita uliofanyika kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida, mabao ya mabingwa hao wa Bara, yalitiwa kimiani na Rama Kipalamoto, Mselemu Salum, Omar Waziri ‘Inzaghi’ na Ramadhani Singano ‘Messi’.
  Simba SC ambayo imewapumzisha wachezaji wake wengi wa kikosi cha kwanza na kuamua kutumia chipukizi waliopandishwa kutoka kikosi cha pili, leo pia ilicheza soka ya kuvutia na kupoteza nafasi kadhaa za kufunga mabao zaidi.
  Kocha Mfaransa, Patrick Liewig alitoa pendekezo la kutolewa kwa wachezaji ‘mafaza’ katika kikosi chake, kwa kuwa hawamsikilizi.
  Miongoni mwa waliotengwa ni wachezaji hodari na vipenzi vya mashabiki kama Amir Maftah, Juma Nyosso, Haruna Moshi ‘Boban’ na Mwinyi Kazimoto.
  Wachezaji hao makinda walicheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu wiki mbili zilizopita dhidi ya Coastal Union ya Tanga na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Sasa timu hiyo inaelekeza nguvu zake katika mechi mbili za kanda ya Ziwa, ikianza na Kagera na baadaye Toto African mjini Mwanza wiki ijayo, huku wapenzi wengi wakiwa na imani na yosso wao hao. 
  Simba itaondoka kesho asubuhi kuelekea Bukoba tayari kwa mechi na Kagera Jumatano. 
  Kwa sasa, Simba SC inashika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu, ikiwa na pointi 34, tatu nyuma ya Azam FC inayoshika nafasi ya pili wakati Yanga SC wapo jirani kabisa na ubingwa kwa pointi zao 48 ligi ikiwa imebakiza mizunguko sita kutia nanga.
  Simba SC inapambana hata kama itapoteza ubingwa, basi iipiku Azam FC katika nafasi ya pili.
  Katika mchezo wa leo, kikosi cha Simba kilikuwa; Abuu Hashim, Emily, Hassan Hassan, Hassan Khatib, Jonas Mkude, Ndemla, Abdallah Sesemea, Rashid Ismail, Christopher Edward, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Haroun Chanongo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: CHRISTOPHER EDWARD AFUFUA MAKALI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top