• HABARI MPYA

  Saturday, March 30, 2013

  AKINA NDITI WAVIPIGA NNE VITOTO VYA WENGER NA KUTINGA FAINALI


  BAO la Lewis Baker katika dakika za nyongeza limeiwezesha timu ya vijana ya Cheslea kushinda mechi ya Nusu Fainali ya michuano ya vijana, NextGen baada ya kuifunga Arsenal mabao 4-3. 
  Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya vijana ya England chini ya umri wa miaka 19, alifunga bao hilo akiunganihsa krosi ya John Swift kutoka wingi ya kulia na kuimaliza Arsenal iliyoongoza mechi hiyo hadi 3-1 katika dakika tano za mwisho za muda wa kawaida.
  Chelsea, ambayo iliongozwa na kiungo Mtanzania, Adam Nditi, sasa itamenyana na Aston Villa katika fainali Jumatatu.
  Mabao mengine ya Chelsea yalifungwa na Feruz na Baker mawili, wakati ya Arsenal yalifungwa na Akpom mawili na Gnabry moja.
  Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Iliev, Bellerin, Hayden, Hajrovic, Angha/Ormonde-Ottewill dk67, Olsson, Ebecilio/Maitland-Niles dk105, Yennaris, Eisfeld/Ansah dk67, Gnabry, Akpom

  ChelseaBeeney; Christensen, Davey, Pappoe, Wright; Loftus-Cheek/T Musonda dk70, Boga/Swift dk75, Baker; Kiwomya, Feruz, Adam Nditi/Hunte dk40.
  Late winner: Chelsea's Lewis Baker scored an extra time winner to earn his team a place in the NextGen final
  Ushindi wa lala salama: Mchezaji wa Chelsea, Lewis Baker (Namba 6) akishangilia bao lake alilofunga katika dakika za nyongeza na kuipeleka timu yake fainali ya NextGen

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: AKINA NDITI WAVIPIGA NNE VITOTO VYA WENGER NA KUTINGA FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top