• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 25, 2013

  SUAREZ ANAWEZA KUTUA BAYERN LICHA YA KLABU KIBAO KUBWA KUMTAKA KWA SABABU WAKALA WAKE NI KAKA WA GUARDIOLA


  KLABU ya Bayern Munich ipo tayari kutumia turufu yake katika njia tatu kumnasa Luis Suarez baada ya kugundulika kwamba, kaka yake Pep Guardiola ndiye mshauri wa mshambuliaji huyo wa Liverpool juu ya mustakabali wake.
  Vyanzo vikuu ndani ya Juventus vimethibitisha nia ya kujiunga katika mbio za kuwania saini ya mchezaji huyo mwenye thamani ya pauni Milioni 40, Suarez, wakati klabu ya zamani ya Guardiola, Barcelona nayo pia iko kwenye kinyang'anyiro hicho.
  Lakini vinara wa Serie A, Juve kwa siri wamekiri Bayern wapo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kushinda marathoni hiyo, kutokana na kaka yake Guardiola, Pere kuwa wakala wa Suarez.
  Race is on: Luis Suarez will be targeted by a number of top clubs this summer
  Mbio zinaendelea: Luis Suarez anawaniwa na kadhaa kubwa Ulaya zimnase mwishoni mwa msimu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SUAREZ ANAWEZA KUTUA BAYERN LICHA YA KLABU KIBAO KUBWA KUMTAKA KWA SABABU WAKALA WAKE NI KAKA WA GUARDIOLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top