• HABARI MPYA

  Wednesday, March 27, 2013

  AZAM NA PRISONS KATIKA PICHA LEO CHAMAZI

  Mshambuliaji Kipre Herman Tchetche akishangilia kwa staili ya Lionel Messi wa Barcelona, baada ya kuifungia Azam FC bao la kwanza kati ya mawili aliyofunga katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Azam ilishinda 3-0.

  Khamis Mcha 'Vialli' akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Prisons 

  Salum Abubakar 'Sure Boy' akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Prisons

  Kikosi cha Azam leo

  Makocha Wasaidizi wa Azam, Muingereza Kali Ongala kushoto na Mkenya Ibrahim Shikanda katika mchezo wa leo

  Wazee wa bench; Kutoka kulia Jabir Aziz, Aishi Manula, Gaudence Mwaikimba na Abdi Kassim aliyeingia kipindi cha pili

  Kiungo wa Azam, Mkenya Humphrey Mieno akipambana na kipa na beki wa Prisons

  Kikosi cha Prisons leo

  Kazi kazi; Humphrey Mieno akipiga mpira kwa staili ya aina yake mbele ya beki wa Prisons, wengine kulia ni Joackins Atudo na John Bocco

  Mchezaji wa Prisons kulia akijaribu kumzibia njia beki wa Azam FC, Joackins Atudo asipande kusaidia mashambulizi 

  Mfungaji wa bao moja la Azam leo, John Bocco kulia akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Prisons

  Kipa wa Prisons, David Burhan akiwa amedaka mpira wa juu mbele wachezaji wa Azam na mabeki wake wakimlinda

  Pati la ushindi; Wachezaji wa Azam wakishangilia moja ya mabao yao leo

  Wachezaji wa Prisons wakimzonga refa kupingana na moja ya maamuzi yake

  John Bocco akiwakimbiza mabeki wa Prisons

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: AZAM NA PRISONS KATIKA PICHA LEO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top