• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 19, 2013

  RASMI MBEYA CITY, ASHANTI NA RHINO ZAPANDA LIGI KUU MSIMU UJAO

  Wachezaji wa Ashanti wakishangilia kupanda Ligi Kuu hivi karibuni baada ya kuifunga Villa Squad

  Na Boniface Wambura
  TIMU tatu zimeshuka daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara kurudi Ligi ya Mkoa msimu ujao wa 2013/2014 baada ya kushika nafasi za mwisho katika ligi hiyo msimu huu 2012/2013 iliyomalizika wikiendi iliyopita.
  Small Kids ya Rukwa imeporomoka kutoka kundi A baada ya kuondolewa kwenye michuano hiyo mapema kwa kushindwa kufika uwanjani kwenye moja ya mechi zake. Kwa mujibu wa kanuni matokeo yote ya mechi ilizocheza yalifutwa.
  Moro United ya Dar es Salaam ndiyo iliyoaga FDL kutoka kundi B baada ya kumaliza mechi zake ikiwa na pointi tatu. Wakati kutoka kundi C timu iliyoshuka ni Morani ya Manyara iliyomaliza ligi ikiwa na pointi kumi na moja.
  Timu zilizopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao wa 2013/2014 ni Mbeya City ya Mbeya iliyoongoza kundi A ikiwa na pointi 31, vinara wa kundi B timu ya Ashanti United ya Dar es Salaam yenye pointi 29 wakati Rhino Rangers ya Tabora imepanda kutoka kundi C ikiwa na pointi 32.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: RASMI MBEYA CITY, ASHANTI NA RHINO ZAPANDA LIGI KUU MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top