• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 18, 2013

  AFRICAN LYON YAZINDUKA, YAUA 1-0 NA SASA YAWEZA BAKI LIGI KUU

  African Lyon; Yapata ushindi kufufua matumaini ya kubaki Ligi Kuu

  Na Prince Akbar
  VIBONDE wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, African Lyon leo wameona mwezi baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Shujaa wa Lyon leo alikuwa ni Benedictor Mwamlagala aliyeifungia timu yake hiyo bao hilo pekee la ushindi dakika ya 14 katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua.
  Kwa ushindi huo, Lyon ambayo ilikuwa inajulikana kama Mbagala Market, sasa imetimiza pointi 15 baada ya kucheza mechi 21, ingawa inaendelea kushika mkia katika Ligi Kuu.
  Lyon sasa angalau unaweza kusema imeanza kupambana kuepuka balaa la kushuka Daraja, ikiwa haizidiwi pointi nyingi sana na timu nne zilizo juu yake, JKT Ruvu yenye pointi 22 nafasi ya 10, Prisons yenye pointi 20 nafasi ya 11, Polisi Moro pointi 17 nafasi ya 12 na Toto African pointi 17 nafasi ya 13. 

  MCHUANO WA KUEPUKA KUSHUKA DARAJA ULIVYO:  
  P W D L GF GA GD Pts
  10 JKT Ruvu 20 6 4 10 19 32 -13 22
  11 TZ Prisons 20 4 8 8 11 17 -6 20
  12 Polisi Moro 21 3 8 10 12 22 -10 17
  13 Toto African 21 3 8 10 17 29 -12 17
  14 African Lyon 21 4 4 13 14 32 -18 15
  Nani atanusurika? 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: AFRICAN LYON YAZINDUKA, YAUA 1-0 NA SASA YAWEZA BAKI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top