Tetesi za J'pili magazeti ya Ulaya


MOYES BORA AACHE KAZI KULIKO MCHEZAJI KWENDA MAN UNITED

KOCHA David Moyes anaweza kubwaga manyanga Everton ikiwa klabu hiyo itaamua kumuuza beki Leighton Baines kwa klabu ya Manchester United.
KLABU ya Real Madrid imeamua kuachana na mchezeshaji wa Manchester City, David Silva na sasa itachuana na Chelsea kuwania saini ya kiungo wa Everton, Marouane Fellaini.
KLABU ya Chelsea inajiandaa kusajili winga wa Anderlecht, Charly Musonda mwenye umri wa miaka 15, ambaye anatabiriwa kuja kuwa tishio katika soka ya Ulaya baadaye.
KIUNGO Mkenya wa Celtic, Victor Wanyama anatarajiwa kuhamishia makali yake katika Ligi Kuu ya England, kutokana na klabu kadhaa za huko kuonyesha nia ya kumsajili kinda huyo wa miaka 20. Habari kamili: Daily Record 

TETESI ZA EURO 2012

KIUNGO wa Ufaransa, Yohan Cabaye anaamini kumbana Steven Gerrard ndio ufunguo wa kuifunga England.
GWIJI wa Arsenal, Ray Parlour amesema Arsene Wenger ni sehemu ya wanaostahili lawama kwa nyota wa Urusi,  Andrey Arshavin kushindwa kung'ara katika klabu hiyo.
GWIJI wa Manchester United, Teddy Sheringham anaamini kukosda matumaini kwa England kunaweza kuwazindua kufanya vizuri katika Euro 2012 kama ilivyokuwa mwaka 1996.
The long wait is finally over for Republic of Ireland's Richard Dunne
Richard Dunne
KOCHA wa Uholanzi, Bert Van Marwijk amekataa kumtupia lawana za kipigo cha Denmark juzi, mshambuliaji wake Robin van Persie aliyecheza chini ya kiwango
KIUNGO Andres Iniesta anaamini kwamba upinzani wa Barcelona dhidi ya Real Madrid lazima uwekwe kando, ikiwa Hispania wanataka iendelee kuwa bingwa wa Ulaya.
NYOTA wa Jamhuri ya Ireland, Richard Dunne amesubiri kwa miaka 10 kucheza michuano ya Euro na timu yake ya taifa.
REDKNAPP HAKAI SPURS
KOCHA wa Harry Redknapp anaweza kuwa karibu kuondoka Tottenham kufuata kazi ya maslahi mazuri Mashariki ya Kati, kutokana na mazungumzo ya mkataba wake mpya Spurs kufeli.
ENGLAND WAKATA TIKETI ZA KURUDI NYUMBANI MAPEMAAAA
CHAMA cha Soka England kimefanya booking ya tiketi za kurejea nyumbani kutoka michuano ya Euro 2012, Juni 20, mwaka huu, siku ambayo watatoka kucheza mechi yao ya mwisho ya Kundi lao.