| Mbwana Samatta kushoto, akimtoka beki wa El Merreikh ya Sudan katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwezi uliopita. Mbwana hivi sasa ni gumzo kubwa na wachezaji wengi wakubwa Afrika, akiwemo Mwanasoka Bora Afrika, Yaya Toure wamesema ana sifa za kucheza klabu kubwa Ulaya. Drogba amesema dogo huyo anaweza hata kurithi jezi yake pale Stamford Bridge. Je, Samatta atatizimiza ndoto zake? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona- lakini jambo la msingi ni yeye kuongeza bidii badala ya kubweteka na sifa hizi. |
0 comments:
Post a Comment