• HABARI MPYA

    Sunday, June 10, 2012

    BAADA YA KUUA NGE, STARS YATAFUTA SUMU YA MAMBA


    Kocha Kim Poulsen akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mechi leo

    KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen amesema baada ya ushindi wa leo dhidi ya Gambia 'Nge' katika mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014, sasa anaelekeza nguvu zake katika mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Msumbji 'Mambas' wiki ijayo mjini Maputo.
    Poulsen alisema amefarijika na ushindi wa leo akiiongoza timu hiyo katika mechi ya tatu tangu aanze kazi, akirithi mikoba ya Mdenmark mwenzake, Jan Borge Poulsen na anaamini sasa ana nafasi ya kucheza Kombe la Dunia 2014 hivyo anajipanga zaidi ili kufanya vizuri.
    Kim aliiambia BIN ZUBEIRY baada ya mechi ya leo, ambayo mabao ya Shomari Kapombe wa Simba na Erasto Nyoni wa Azam kipindi cha pili yaliifanya Stars itoke nyuma kwa 1-0 na kushinda 2-1 dhidi ya Gambia kwamba kesho timu inaanza mazoezi kujiandaa na mechi na Msumbiji.
    Poulsen amewataka vijana wake kutolewa sifa na badala yake kuelekeza nguvu zao katika maandalizi ya mechi ijayo dhidi ya  Msumbiji, kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika mwani Afrika Kusini.
    Katika mchezo wa kwanza, Stars wakati bado inanolewa na Jan Poulsen ililazimishwa sare ya 1-1 na Msumbiji nyumbani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BAADA YA KUUA NGE, STARS YATAFUTA SUMU YA MAMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top