• HABARI MPYA

    Thursday, April 05, 2012

    YOUN MUSLIM WAPANIA KUFANYA MAKUBWA NAIROBI


    TIMU ya soka ya Young Muslim imeondoka jijini Dar es Salaam leo kuelekea Nairobi, Kenya kushiriki mashindano ya Sunni Muslim Football Tournament yanayotarajiwa kuanza kesho mjini humo.

    Akizungumza kabla ya kuondoka, Meneja wa timu hiyo Salim Issak alisema kuwa mashindano hayo yanahusisha timu zilizopo chini ya Jumuiya Muslim Janat kutoka miji ya Dar es Salaam, Arusha, Zanzibar na Mombasa.

    Alisema kuwa kikosi chake kimejiopanga vema kuhakikisha kinashinda michuano hiyo yenye lengo la jumuiya hizo, inatarajiwa kumalizika Aprili 9.

    Aliongeza kuwa msafara wa watu 25 wakiwemo viongozi watano na wachezaji 20 umeondoka chini ya udhamini wa Nitak, Muza Oil Mills, Arif Khatri na Kilombero Sugar.

    Bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni timu ya Mombasa ambapo timu Young Muslim ilitwaa kombe hilo kwa mara ya mwisho mwajka 2010 katika michuano iliyofanyika Visiwani Zanzibar.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YOUN MUSLIM WAPANIA KUFANYA MAKUBWA NAIROBI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top