![]() |
| Perez |
BAO la Hernan Perez dakika za
majeruhi usiku wa jana, liliipa Villarreal ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Malaga,
ushindi ambao unawaongezea matumaini ya kutoshuika daraja La Liga.
Timu hiyo ambayo inajulikana
kama 'The Yellow Submarine', ambayo inashika nafasi ya 17, imefikisha pointi
saba kamili za kuwaweka salama kutoka eneo la hatari, baada ya kufikisha pointi
35 zikiwa zimebaki mechi sita.
Villarreal ilimaliza katika
nafasi ya nne msimu uliopita na kucheza Ligi ya Mabingwa, lakini imeshuka mno msimu
huu na sasa ina kocha wa tatu kwa msimu huu mmoja pekee, Miguel Angel Lotina anayejaribu
kuiepusha na balaa la kushuka daraja.
Kiungo wao wa Paraguay, Perez alifunga
bao dakika ya 94 kuiwezesha kuchukua pointi hizo, katika mchezo ambao kipa wa Malaga,
Mcameroon Carlos Kameni alilimwa kadi nyekundu dakika ya 81.
Kipa huyo wa Cameroon,
alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumuangusha Perez kwenye eneo la
hatari na Marcos Senna akafunga la kusawazisha kwa penalti.
Mwanasoka wa kimataifa wa Hispania,
Santi Cazorla, aliyekuwa chachu ya mafanikio ya Villarreal msimu uliopita,
aliifungia bao la kuongoza Malaga dakika ya 65, lakini hakushangilia kukwepa
kuwaudhi mashabiki wa timu yake ya zamani.
Malaga, ambayo inamilikiwa na
mtu wa Qatari, inabaki nafasi ya nne kwa pointi zake 50 na imeshindwa kuipiku
Valencia yenye pointi 52 katika nafasi ya tatu. Valencia iliifunga Rayo
Vallecano 4-1 juzi.



.png)
0 comments:
Post a Comment