![]() |
| Marehemu Kanumba |
MTANDAO wa wasanii Tanzania
(SHIWATA) umeandaa ibada maalum ya kumwombea aliyekuwa muigizaji wa filamu
nchini, marehemu Steven Kanumba itakayofanyika Jumapili Aprili 15, 2012 kwenye
ukumbi wao wa Ilala, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Shiwata, Kassim
Taalib amesema leo kuwa amewaomba wanachama wote wahudhurie ibada hiyo ambayo
ni moja ya matukio ya mtandao huo katika kuwaombea wanachama waliofikwa na vifo
akiwemo mwanachama wao Kanumba aliyeshiriki kwa ukamilifu, uadilifu na mchango
mkubwa katika shirikisho hilo katika harakati za kujikomboa kiuchumi.
Alisema Kanumba ambaye alikuwa
mwanachama wa Shiwata alikuwa mchapakazi, mpenda maendeleo na aliyewahi
kushiriki kikamilifu katika kutafuta mashamba na maeneo ya makazi ambako
alikwenda Bagamoyo, Kisarawe na hatimaye kufanikiwa kupata eneo wilayani
Mkuranga mkoa wa Pwani, katika mashamba hayo wanachama zaidi ya 1,000
wamefanikiwa kupata maeneo ya makazi marehemu Kanumba akiwa mmojawapo.
Alisema Shiwata inakusudia
kujenga makumbusho makubwa ya wasanii waliofariki wakiwa katika harakati za
kuendeleza kazi za wasanii katika kijiji cha Mwanzega.
"Katika makumbusho hayo pia
zitawekwa kumbukumbu za kazi za sanaa ikiwemo ya Waziri Mkuu wa zamani
marehemu, rashida Kawawa aliyeacheza sinema ya Muhogo Mchungu pamoja na wengine
kama marehemu Fundi Saidi (Mzee Kipara),wasanii 13 wa Five Stars na
Kanumba"alisema Talib.
Aliongeza kuwa Shiwata pia inakusudia kuandaa mashindano ya sanaa ya vikundi
mbalimbali wakianzia mkoa wa Dar es salaam, mashindano kama hayo yaliwahi
kufanyika mwaka 2003 kati ya vikundi vya Kaole,Splendid, Savanna, Nyota
Academia,Mambo hayo, Kidedea,Black Eagle na kuibua vipaji mbalimbali akiwemo
Cheni, Muhogo Mchungu na marehemu Kanumba.
Lengo la mashindano hayo ni
kuinua vipaji vya wasabii wa bongo Flava, Sarakasi, filamu, ngoma, taarabu na
muziki wa dansi.



.png)
0 comments:
Post a Comment