• HABARI MPYA

    Thursday, April 12, 2012

    DEL PIERO AIRUDISHA KILELENI JUVE AKICHEZA MECHI YA 700

    Del Piero kulia
    KLABU ya Juventus imerejea kileleni mwa Serie A baada ya Alessandro Del Piero kufunga bao la dakika za lala salama akicheza mechi ya 700 na kuiongoza klabu yake kushinda 2-1 nyumbani dhidi ya usiku huu.
    AC Milan iliifunga Chievo 1-0 jana na kurudi kileleni kwa tofauti ya pointi mbili, lakini Juve sasa inaongoa tena kwa tofauti ya pointi moja.
    Awali, Lazio ilisawazisha kupitia kwa  Stefano Mauri baada ya Simone Pepe kufunga la kuongoza.
    Katika mechi nyingine, AS Roma iliwafunga Udinese 3-1 wakati Napoli imefungwa 3-1 na Atalanta na Inter Milan imeifunga Siena 2-1, shukrani kwake Diego Milito aliyefunga mawili San Siro.
    Cesena imetoka 1-1 na Genoa, Novara imefungwa 2-0 na Parma, Lecce imeifunga 2-1 Catania
    Inter sasa inalingana na Napoli katika nafasi ya mwisho ya kuwania kucheza Europa League, huku kocha wake mpya, Andrea Stramaccioni akishinda mechi ya pili katika mechi tatu tangu aanze kazi na Napoli inashindwa kushinda kwa mara ya tano mfululizo kwenye ligi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DEL PIERO AIRUDISHA KILELENI JUVE AKICHEZA MECHI YA 700 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top