TIMU ya Brazil imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Fainali za Kombe la Dunia baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Japan usiku wa jana Uwanja wa NRG Jijini Houston, Texas nchini Marekani.
Haukuwa ushindi mwepesi kwa mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia baada ya kutanguliwa kwa bao la dakika ya 29 la kiungo wa Mainz 05 ya Ujerumani, Kaishu Sano.
Mabao yote ya Brazil yamefungwa na nyota kutoka Ligi ya England, kiungo wa ulinzi, Carlos Henrique Casimiro wa Manchester United dakika ya 57 na mshambuliaji wa Arsenal, Gabriel Teodoro Martinelli Silva dakika ya 90’+5.



.png)
0 comments:
Post a Comment