• HABARI MPYA

  Thursday, February 18, 2016

  REFA AKATAA BAO LA ULIMWENGU MAZEMBE YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA ST ELOI LUPOPO

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu (pichani kushoto) amefunga bao la kichwa leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), lakini likakataliwa TP Mazembe ikitoa sare ya bila kufungana na FC Saint Eloi Lupopo.
  Ulimwengu maarufu kama Rambo mbele ya mashabiki wa Tout Puissant Mazembe, ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – OINLINE  kwa simu usiku wa Jumatano kwamba ni kweli alifunga akiwa ameotea Uwanja wa Frederic Kibassa Maliba mjini Lubumbashi.
  “Ndiyo, ni kweli niliingia kwenye mtego wa kuotea, wakati nafunga, ulikuwa mchezo mgumu, tumetoa sare ya 0-0 kwenye Uwanja wao wao, lakini hapa hapa Lubumbashi,”amesema Ulimwengu.
  Baada ya mchezo huo Ulimwengu na Mazembe – wafalme wa Ligi ya Mabingwa Afrika, wanarejea kambini kujiandaa na mchezo wa Super Cup ya Afrika dhidi ya mabingwa wa Kombe la Shirikisho, Etoile du Sahel ya Tunisia.
  “Sasa tunaelekea kwenye maandalizi ya Super Cup, mchezo ambao utachezwa Jumamosi kwenye Uwanja wetu (wa Mazembe). Nina kiu ya taji hilo, naomba Mungu atusaidie tulichukue,”amesema. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA AKATAA BAO LA ULIMWENGU MAZEMBE YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA ST ELOI LUPOPO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top