• HABARI MPYA

    Tuesday, February 16, 2016

    KOCHA WA TIMU YA TAIFA ZAMBIA AFARIKI DUNIA

    FAMILIA ya soka Zambia imepatwa na msiba, kufuati kifo cha kocha wa timu ya Olimpiki, Fighton Simukonda (pichani kushoto).
    Simukonda amefariki jana asubuhi, Februari 15, 2016 katika hospitali ya Konkola Mine mjini Chililabombwe, alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa kisukari katika ya kutimiza miaka 58 ya kuzaliwa.
    Moja ya kazi za kukumbukwa hivi karibuni ni alipoiongoza timu ya taifa ya Zambia chini ya umri wa miaka 23 kwenye Fainali za Afrika nchini Senegal mwezi Desemba mwaka jana, ambako Chipolopolo ilitolews hatua ya makundi.
    Simukonda alikuwa kocha wa kwanza mzalendo kuifikisha klabu ya Zambia katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2009 akiwa na Zesco United. 
    Alitwaa mataji matatu ya ligi, akiwa na Zanaco mawili mwaka 2005 na 2006 na moja akiwa na Zesco United mwaka 2010 na pia alishinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka Zambia mara tatu katika miaka ya 2005, 2009 na 2010.
    Alikuwa kazini pia wakati Chipolopolo inatwa Kombe la COSAFA mwaka 1998.
    Beki huyo, enzi zake anacheza alikuwa miongoni mwa kizazi cha dhahabu cha Nkana ambacho kilitwaa mataji matano ya ligi miaka ya 1980. Wakati fulani pia alikuwa Nahodha wa timu ya taifa ya Zambian. 
    Licha ya kuchezea timu za Zambia kama Mimbula Diggers, KB Davies na Vitafoam United, pia alichezea Jomo Cosmos na Blackpool za Afrika Kusini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA WA TIMU YA TAIFA ZAMBIA AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top