• HABARI MPYA

  Friday, February 12, 2016

  HATIMAYE ATC YAWAPAISHA YANGA SC MAURITIUS BAADA YA MSOTO WA KUTWA NZIMA

  Hatimaye ndege ya Shirika la Tanzania (ATC) imepaa majira ya Saa 1:00 usiku kwa safari ya saa nne angani kwenda na kikosi cha Yanga SC nchini Mauritius ambacho kesho kitamenyana na wenyeji, Cercle de Joachim katika katika mchezo kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuanzia Saa 9:30 Alasiri kwa saa za Mauritius, Uwanja wa Curepipe mjini Curepipe. Yanga SC ilitarajiwa kuondoka Alfajiri ya leo, lakini imelazimika kuondoka usiku huu kutokana na ndege hiyo kuwa inafanyiwa marekebisho baada ya kubainika hitilafu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HATIMAYE ATC YAWAPAISHA YANGA SC MAURITIUS BAADA YA MSOTO WA KUTWA NZIMA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top